Katiba Mpya: Warioba aiumbua CCM

Katiba Mpya: Warioba aiumbua CCM

BAK

JF-Expert Member
Joined
Feb 11, 2007
Posts
124,790
Reaction score
288,165
Warioba aiumbua CCM
• Asema muswada uliopitishwa bungeni unalenga kuifuta tume yake

na Irene Mark
Tanzania Daima

MWENYEKITI wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Jaji mstaafu Joseph Warioba, amesema Muswada wa Sheria ya Marekebisho ya Sheria ya Mabadiliko ya Katiba wa mwaka 2013 uliopitishwa na Bunge hivi karibuni unalenga kuifuta tume hiyo kabla ya kumaliza muda wake.

Muswada huo ambao ulipitishwa na wabunge wa CCM pamoja na Augustine Mrema wa TLP (Vunjo), ulisusiwa na wabunge wa CHADEMA, CUF na NCCR-Mageuzi kutokana na kuchakachuliwa baadhi ya vipengele huku Zanzibar ikiwa haijashirikishwa.

Akizungumza na waandishi wa habari jana jijini Dar es Salaam, Jaji Warioba alisema miongoni mwa vipengele vilivyofanyiwa marekebisho kwenye sheria hiyo ni kile kinachotaka tume yake ivunjwe baada ya kuanza kwa Bunge la Katiba.
Hoja za Warioba ndizo hizo zinazopigiwa kelele na vyama hivyo vitatu pamoja na makundi ya asasi za kiraia huku viongozi wa serikali na Chama Cha Mapinduzi (CCM), wakiwabeza na kudai muswada huo ulipitia taratibu zote.

Alisema marekebisho hayo yanakwenda kinyume cha sheria mama iliyounda tume hiyo ambayo inaweka wazi kwamba majukumu ya tume yatafika ukomo baada ya kupigwa kura ya maoni.
Kwa mujibu wa Jaji Warioba, uamuzi wa wabunge hao utaleta mkanganyiko endapo watashindwa kuelewana kwenye baadhi ya vipengele, kwani hapatakuwa na mtu wa kuwafafanulia, kwa kuwa tayari tume itakuwa imevunjwa.

“Sheria iliyounda tume hii inasema wazi kwamba ukomo wa tume ni baada ya wajumbe wa tume hiyo kutoa elimu kwa umma kuhusu kura ya maoni na mchakato wa kupiga kura hiyo utakapokamilika.
“Wao hawaoni sababu ya sisi kuendelea kuwapo hapa, nawaomba watafakari kipengele hicho,” alisema Warioba aliyepata kuwa waziri mkuu wa Tanzania.


Kabla ya kuhitimishwa kwa mkutano wa 12 wa Bunge mjini Dodoma, wabunge wa upinzani walitoka nje wakisusia kupitishwa kwa mabadiliko ya sheria hiyo, wakidai kufutwa kwa baadhi ya vipengele vilivyobadilishwa dakika za mwisho bila kuwahusisha.
Kususa huko wakati kikao kinaendelea kuliambatana na vurugu baada ya Naibu Spika, Job Ndugai, kuwataka askari wa Bunge kumtoa nje Kiongozi wa Kambi ya Upinzani, Freeman Mbowe, jambo lililowafanya wabunge wa vyama hivyo vitatu kutoka wote.

Pamoja na madai hayo, wabunge hao walilalamikia utendaji wa Kamati ya Bunge inayoshughulikia Katiba na Sheria chini ya uenyekiti wa Mbunge wa Viti Maalumu, Pindi Chana, kwa kubadili vipengele hivyo kabla ya kuupitisha bungeni.
Baada ya wabunge wa upinzani kususa, wabunge wachache wa CCM waliokuwapo ukumbini hapo na Mrema, walipitisha mabadiliko hayo na kuyapeleka kwa rais ili asaini na kuifanya kuwa sheria.

Nje ya Bunge
Moto uliowashwa nje ya Bunge na viongozi wa upinzani pamoja na makundi ya asasi za kiraia umebadili upepo kwani kelele za kumtaka Rais Jakaya Kikwete kutousaini muswada huo zimezidi kuongezeka.
Ni katika hatua hiyo, mawaziri kadhaa, William Lukuvi wa Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu na Bunge), Stephen Wasira na Mathias Chikawe wa Katiba na Sheria, wamekuwa wakiendelea kuwabeza wapinzani.

Hivi karibuni Waziri Chikawe alifikia hatua ya kumtisha Rais Kikwete akisema kuwa endapo hatausaini muswada huo kuwa sheria atakuwa ametangaza mgogoro na Bunge.
Pia Wasira naye amenukuriwa akisema kuwa wanaopinga muswada huo usisainiwe lazima wampe rais sababu za kutofanya hivyo, kwa vile hana, na kwamba milango ya Ikulu kwa wapinzani hao kujadiliana na mkuu wa nchi imefungwa
.


Matamshi hayo ndiyo yamewaleta pamoja viongozi wa vyama hivyo na makundi mengine wakizunguka kwa wananchi kuwaeleza karoso zilizomo kwenye muswada huo ambao CCM inataka kutumia turufu hiyo kuhodhi mchakato wa Katiba mpya.

Angalizo la Warioba
Mwenyekiti huyo aliwataka wanasiasa kuacha malumbano katika mchakato wa upatikanaji wa Katiba mpya, huku akikanusha uvumi kwamba baadhi ya wajumbe wa tume hiyo wametishia kujiuzulu.
Badala yake aliwataka waketi pamoja na kukubaliana kuhusu vipengele wanavyotofautiana kwenye rasimu hiyo, kisha kuwaeleza wananchi manufaa ya kuwa na Katiba ya wote.

“Huu si wakati wa Tanzania kutengana, wanasiasa wanapaswa kutumia fursa walizonazo kukaa pamoja na kushirikiana ili tupate Katiba bora, hatuwezi kupata Katiba kwa maandamano, mikutano na mivutano baina ya vyama vya siasa,” alisema.
Kwa mujibu wa jaji huyo, kilichopo kwenye rasimu hiyo ni maoni ya wananchi, hivyo hakuna haja ya kubadili, bali kuboresha ili kila Mtanzania anufaike na uwepo wa Katiba hiyo.

Alifafanua kuwa kuna baadhi ya wajumbe wa mabaraza walidiriki kuwakashifu wajumbe wa tume yake, hasa kutokana na wanasiasa kutoa matamshi ya kuwalenga wajumbe hao wa tume.
“Hilo limetusikitisha, matamshi hayo yalitolewa kwa lengo la kuwadhalilisha wajumbe wa tume na kuishushia thamani kazi kubwa wanayoifanya ndani ya tume,” alisema.
Jaji Warioba alisema pamoja na changamoto hizo, tume ilifanikiwa kukamilisha mchakato huo ambapo kwa kupitia mikutano 179 ambayo ilihudhuriwa na wajumbe 19,337 wa mabaraza ya Katiba walipata maoni.
Mbali na hatua hiyo, Jaji Warioba alisema tume imepokea maoni kutoka kwa makundi, asasi na taasisi mbalimbali 600 kuhusiana na rasimu ya Katiba mpya.

Alisema baada ya kukusanya maoni hayo, tume inatarajia kuanza mchakato wa kuchambua ili kuandaa ripoti itakayokuwa na maboresho na kuikabidhi kwa rais kwa ajili ya kuendelea kwa mchakato mwingine.
“Tumewahoji wawakilishi wa wananchi kutoka sehemu mbalimbali za Tanzania Bara na Visiwani, zaidi ya vikundi 176 vyenye uwakilishi wa watu tofauti tulikusanya maoni yao.
“Naamini Watanzania wanataka Katiba inayoheshimu utu wa mtu, umoja na kuvumiliana,” alisisitiza Jaji Warioba.


 
Safi sana Warioba endelea kua na msimamo kwa manufaa ya Taifa lako wala usiyumbishwe na magamba,hili Taifa sio la ccm,ni Taifa la watanzania kwa hiyo tunaangalia masilahi ya Watanzania na sio chama au kikundi cha majambazi,mafisadi,majangiri na wauaji wa ccm

Sent from my BlackBerry 9300 using JamiiForums
 
Safi sana Warioba endelea kua na msimamo kwa manufaa ya Taifa lako wala usiyumbishwe na magamba,hili Taifa sio la ccm,ni Taifa la watanzania kwa hiyo tunaangalia masilahi ya Watanzania na sio chama au kikundi cha majambazi,mafisadi,majangiri na wauaji wa ccm

Sent from my BlackBerry 9300 using JamiiForums

Kumbe kuna wakati huwa unaona eeeh!?
Kwa hili tuko Pamoja sana mkuu..
 
Jaji Warioba asijisahaulishe kuwa sheria hiyo hiyo imeweka ukomo wa kipindi cha miezi 18 ya tume yake kuvunjwa tangu kuundwa kwake.
 
Tanzania Daima ni gazeti la UDAKU...

As you know all nature is insufficient... sasa Unasoma Magazeti gani? Usiniambie ni UHURU na MZALENDO
Hii ni TOPIC ya Nne naona Unaandika the same thing hata kama sio hilo GAZETI kuna CHUKI sehemu fulani ya MWILI wako kuhusu hilo GAZETI?

Kwasababu kama Unasema ni UDAKU Prove your POINT... we are in 21st CENTURY no GAMES be REAL and TRUSTWORTHY...
 
Wewe ndio wale wale wachumia tumbo, mnaotetea kisichostahili kutetewa na hivyo kuisaliti nchi yenu na Watanzania wenzenu kwa ujira mdogo sana. Haya punda wa mafisadi, majangili, magaidi na wauza unga ndani ya chama chenu, pita Lumumba baadaye leo ukachukue posho yako ya buku 7.

Jaji Warioba asijisahaulishe kuwa sheria hiyo hiyo imeweka ukomo wa kipindi cha miezi 18 ya tume yake kuvunjwa tangu kuundwa kwake.
 
Maccm yatakuwa yanamchukia sana warioba, kisa kaweka mawazo ya wananchi kwenye rasimu ya katiba mpya! Kuna wanaccm wamepanga kumvuruga rais kikwete kuhusiana na mchakato wa kupata katiba mpya! Warioba kaza kamba umsaidie rais kikwete ili atimize matarajio yake...
 

As you know all nature is insufficient... sasa Unasoma Magazeti gani? Usiniambie ni UHURU na MZALENDO
Hii ni TOPIC ya Nne naona Unaandika the same thing hata kama sio hilo GAZETI kuna CHUKI sehemu fulani ya MWILI wako kuhusu hilo GAZETI?

Kwasababu kama Unasema ni UDAKU Prove your POINT... we are in 21st CENTURY no GAMES be REAL and TRUSTWORTHY...

Mkuu,jahazi lazama .. Kutapatapa ndio sehemu ya maisha yao..
Mwanahalisi wamefanikiwa kulizima.. JF na TZ Daima hawawezi katu kudhibiti..wamejitahidi saana kuanzisha VIJARIDA dhidi ya TZ Daima.. lakini hatudanganyiki kwani Ta ya Kijani inatupa Ruksa kusonga Mbele...
 
Mh Warioba tunakupongeza kwa msimao uliotuonyesha Mungu azidi kukupa afya njema ili uone jinsi nchi inavyokombolewa kutoka kwa wakoloni weusi.
 
Mkuu,jahazi lazama .. Kutapatapa ndio sehemu ya maisha yao..
Mwanahalisi wamefanikiwa kulizima.. JF na TZ Daima hawawezi katu kudhibiti..wamejitahidi saana kuanzisha VIJARIDA dhidi ya TZ Daima.. lakini hatudanganyiki kwani Ta ya Kijani inatupa Ruksa kusonga Mbele...
na sasa wanaliwinda mtanzania.kwa makala ya serikali kunuka damu
 
Warioba,vizazi vijavyo vitakukumbuka daima,Endelea kutetea Taifa lako ambalo kwa sasa liko chini ya baba wa Kambo..!
 
- Source ni Tanzania Daima, halafu Warioba anazidi kujichafua kwa sababu kazi ya tume imeisha tayari sasa

Le Mutuz
 
- Source ni Tanzania Daima, halafu Warioba anazidi kujichafua kwa sababu kazi ya tume imeisha tayari sasa analia lia nini?

Le Mutuz

We kweli kazi ipo, harafu unataka ubunge. Kwa staili ya watu kama wewe Tanzania tuna kazi kubwa.Mungu atuepushe na watu kama wewe.
 
We kweli kazi ipo, harafu unataka ubunge. Kwa staili ya watu kama wewe Tanzania tuna kazi kubwa.Mungu atuepushe na watu kama wewe.

- Lets say ninataka ubunge eti unatolewa kwa kuandika jamiiforums? ha! ha! ha! nani amepewa ubunge na jamiiforums? ha! ha!

Le Mutuz
 
na sasa wanaliwinda mtanzania.kwa makala ya serikali kunuka damu

CDM kama upepo.. hiwezi kuzuia popote..
Ukifunga Gazeti,Mijadala itarindima kupitia vijiwe na Blogs.... Mguu kwa Mguu hadi wajue ni namna gani Wenye Tanganyika yao walivyo Watata!
 
- Source ni Tanzania Daima, halafu Warioba anazidi kujichafua kwa sababu kazi ya tume imeisha tayari sasa analia lia nini?

Le Mutuz

Hivi ni lini utakua? Au kwa vile bado unamtegemea baba yako ndio maana unajiona mtoto? Huna busara ktk umri huu. Ulipokuwa kijana ulikuwa mwehu kabisa. Kuna tatizo ktk ubongo wako.
 
Tume nyingi zikiundwa huwa zina hadibu rejea zao na wakimaliza kazi huwa wana pa kukabidhi ripoti zao kisha huenda kulala wakiacha huko walikokabidhi waendelee na waendelelealo nalo.Lakini naona kutwa kiongozi wa tume yuko vyombo vya habari kulikoni?
 
- Source ni Tanzania Daima, halafu Warioba anazidi kujichafua kwa sababu kazi ya tume imeisha tayari sasa analia lia nini?

Le Mutuz

kuna siku ulialikwa startv, uliongea kama mtu mwenye akili (ilikua mara ya kwanza nakusikia live), ilikua ni wakati ule unasema umejitoa jf (kitu ulichoshindwa kufanya hadi leo)

nilikua nashangaa kwa nini raia hawakuelewi, ninavozidi kusoma post zako ndio ninavyozidi kujua ni kwa kiasi gani wewe ni mwepesi upstairs
 
Back
Top Bottom