Hivi ndugu yangu Charity, nani kakwambia CHADEMA wanatunga katiba ya kuendesha nchi?
CHADEMA inachofanya ni shinikizo la kuonesha kuwa kuna haja ya kuwepo kwa katiba mpya kutokana na hii iliyopo sasa kuwa na mapungufu mengi.
Ndio maana ofisi za bunge hawakupeleka katiba, walichopeleka ni motion ya kutaka bunge kujadili na kuona haja ya kupitisha mchakato wa uanzishwaji wa uundwaji wa katiba mpya.
Pia inaonekana hufuatilii kauli za unaowahukumu. mara zote wanaongelea mchakato wa uundwaji wa katiba mpya, TENA KATIBA ITAKAYOUNDWA NA WATANZANIA WENYEWE kwa kuwa iliyopo sasa iliundwa na kakikundi ka watu wa chache na si watanzania wenye nchi.
FUATILIA KABLA YA KUANDIKA KITU ILI USIONEKANE WA AJABU. Ni ushauri wangu kwako!