Mkutano wa halmashauri kuu ya Ccm umemalizika usiku wa manane leo hii. Mkutano huo ulikua ukijadili pamoja Rasimu mpya ya Katiba chini ya Jaji Joseph Warioba!
Msemaji mkuu wa Ccm Nape Nauye akihojiwa na Mtangazaji wa BBC Daved Nampesia,alisema kua Ccm watatoa tamko la Chama leo mchana juu ya nini msimamo wao kwa Rasimu hiyo ya Katiba Mpya.
Hii ni wazi kuwa Ccm hawakufurahishwa na Rasimu hii ya Katiba mpya chini ya Jaji Warioba haswa ktk vipengele viwili. Kipengele cha Mgombea binafsi na kile cha Muundo wa serikali tatu. Ndio maana ccm wameweweseka na kuamua kujadili swala hili ktk mkutano wao mkuu.
Imekua ni kawaida kwa ccm kupinga kile kinacho kubalika na vyama vya upinzani huku ikikubali kile kinachopingwa na Vyama vya upinzani. Rasimu ya Katiba mpya ni MAONI ya Watanzania na sio maoni ya Tume wala Vyama! Inashangaza Ccm kupinga MAONI ya Wananchi huku wakijisahau kuwa hata wao wamepewa uongozi na hao hao Wananchi.
CCM imejikuta ktk wakati mgumu kwa kuwa tangia mwanzo wa kuunda Tume wamekua wakijitahidi kuhakikisha kwamba tume hiyo inakua chini yao na kuwa maoni ambayo yangewasilishwa yangekua ya wana ccm na sio Wananchi.
Balozi wa Marekani nchini Tanzania akizungumza jana alisema kuwa vyama na wanaharakati lazima waheshimu matakwa ya Wananchi kwa kuwa ndio Demokrasia.
Je Ccm kutaka kupinga Maoni ya Watanzania kwa vile tu inaingilia Masilahi yao Kisiasa haswa kwa kipengele cha Mgombea Binafsi ni DEMOKRASIA?
mkuu kama kupotosha ni taaruma yako tuambie,lini na wapi ccm wamepinga rasimu ya katiba kama siyo kudanganya watu,ndiyo kwanza ccm wamekaa jana ili waijadili rasimu kama tunavyojadili mimi na wewe na wakati ukifika wataenda kutoa maoni yao kwenye tume na lazima ukumbuke kuwa hii siyo katiba bali ni rasimu hivyo itaendelea kuboreshwa kutokana na maoni yatakayotolewa na watanzania.