Katiba Mpya Yaiva: Kikwete na Shein kukabidhiwa ripoti Disemba 30, 2013

Katiba Mpya Yaiva: Kikwete na Shein kukabidhiwa ripoti Disemba 30, 2013

Status
Not open for further replies.

Mwalwimle

Member
Joined
Oct 19, 2011
Posts
9
Reaction score
0
TUME YA MABADILIKO YA KATIBA

Hafla ya kukabidhi Rasimu ya Katiba kwa Mhe. Rais
Tume ya Mabadiliko ya Katiba inapenda kuwafahamisha wananchi na wadau wengine wote kuwa Hafla ya kukabidhi Rasimu ya Katiba kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe, Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete na Mhe. Dkt. Ali Mohammed Shein, Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi itafanyika siku ya Jumatatu, Desemba 30, 2013 katika Viwanja vya Karimjee, jijini Dar es Salaam.Hafla hiyo pia inatarajiwa kuhudhuriwa na viongozi wa Serikali, vyama vya siasa, taasisi za kidini, asasi za kiraia na wananchi wa kawaida.

Taarifa zaidi kuhusu hafla hii zitatolewa baadaye.
Imetolewa na:Assaa Rashid, Katibu, Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Dar es Salaam, Alhamisi, Desemba 19, 2013
 
Wakabidhi tu maana wasitumalizie wajumbe bure, mpaka sasa tumewazika tayari wajumbe wawili Dr.Mvingi na yule jaji Ernest Mwapopo
 
safi sana katiba mpya hiyooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooo yaja.
 
TUME YA MABADILIKO YA KATIBA
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI


Hafla ya kukabidhi Rasimu ya Katiba kwa Mhe. Rais

Tume ya Mabadiliko ya Katiba inapenda kuwafahamisha wananchi na wadau wengine wote kuwa Hafla ya kukabidhi Rasimu ya Katiba kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe, Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete na Mhe. Dkt. Ali Mohammed Shein, Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi itafanyika siku ya Jumatatu, Desemba 30, 2013 katika Viwanja vya Karimjee, jijini Dar es Salaam.

Hafla hiyo pia inatarajiwa kuhudhuriwa na viongozi wa Serikali, vyama vya siasa, taasisi za kidini, asasi za kiraia na wananchi wa kawaida.

Taarifa zaidi kuhusu hafla hii zitatolewa baadaye.


Imetolewa na:
Assaa Rashid,
Katibu,
Tume ya Mabadiliko ya Katiba,
Dar es Salaam,
Alhamisi, Desemba 19, 2013
 
Asante kwa taarifa hii muhimu kwa minaajili ya mustakabali wa taifa letu.
 
Wananchi walizungumzia sana suala la ardhi lakini kwenye Rasimu halipo. Sijui ni kwa sababu gani?
 
Wananchi walizungumzia sana suala la ardhi lakini kwenye Rasimu halipo. Sijui ni kwa sababu gani?

Sheria ya ardhi ina kurasa elfu mbili, bado mnataka kuweka ardhi katika Katiba badala ya kwenda kutafuta kwa nini hakuna utii wa sheria? Hiyo Katiba ndiyo mtaiheshimu na kuifuata wakati Morogoro watu wanauwana? Dr. Harrison Mwakyembe anakwenda kukwamua abiria wasilanguliwe nauli anaitwa JEMBE. Au na nauli za mabasi ziingizwe katika rasimu ya Katiba. WaTz hawajui hata matatio yao yalianzia wapi, imebaki ahadi ya dawa katika Katiba Mpya.

Ulaya wamekwishaanza kuandika hivi:"Tanzania ni Jamhuri ya Zanzibar Mjini." (Tanzania, United Republic of Zanzibar Urban). Ukitaka nikuonyeshe lilipo hilo Jogoolashamba nitakuonyesha Walahi Ladhim! .
 
what I don't understand ni kwanini kuna sherehe na halfa za aina hii... nilidhani sherehe ya maana ingefanyika wananchi wanapopata Katiba Mpya... sasa kila draft inafanyiwa halfa?
 
what I don't understand ni kwanini kuna sherehe na halfa za aina hii... nilidhani sherehe ya maana ingefanyika wananchi wanapopata Katiba Mpya... sasa kila draft inafanyiwa halfa?

mkuu wamekubakisha ww, angalia yasije kukuta kama ya mwagosi!!
 
Tume ya Mabadiliko ya Katiba inatarajiwa kuwakabidhi Marais Jakaya Kikwete na Dk Mohamed Shein, rasimu ya katiba mpya.


Hafla ya makabidhiano hayo itafanyika Jumatatu, kwenye viwanja vya Karimjee, jijini Dar es Salaam.

Taarifa iliyotolewa jana jijini Dar es Salaam na Katibu wa Tume, Assaa Rashid, ilisema.
Akitoa ufafanuzi kuhusu kuendelea kuwepo kwa tume hiyo, Naibu Waziri wa Sheria na Katiba, Angela Kairuki, alisema tume itakabidhi nyaraka hizo na itaendelea na kazi.


Alisema itavunjwa kwa mujibu wa sheria baada ya rasimu hiyo kufikishwa na kusomwa kwenye Bunge Maalum la Katiba.


Taarifa ya Rashid ilieleza kuwa hafla hiyo pia inatarajiwa kuhudhuriwa na viongozi wa serikali, wa kisiasa, taasisi na asasi mbalimbali zikiwamo za kidini na kiraia pamoja na wananchi.
Taarifa hiyo ilisema Mwenyekiti wa Tume, Jaji Joseph Warioba, anatarajia kuwakabidhi Marais, ripoti ya mchakato pamoja na rasimu ya katiba mpya.


Rasimu hiyo imetokana na maoni ya wananchi, viongozi na makundi mbalimbali waliyoyawasilisha kwa tume kupitia njia mbalimbali zikiwamo mikutano ya hadhara, barua pepe, njia ya posta, tovuti (Tume ya Mabadiliko ya Katiba) na ukurasa wa facebook wa tume (Tume ya Mabadiliko ya Katiba Tanzania) na mabaraza ya katiba.
Mchakato wa kupata katiba mpya ulianza Julai, mwaka jana baada ya kuundwa kwa sheria ya kuanzisha tume ya mabadiliko ya katiba.


Kwa mujibu tangazo la Rais Kikwete kuhusu kuandikwa katiba mpya Tanzania inatarajia kuwa na katiba mpya ifikapo Aprili 2014, wakati wa maadhimisho ya miaka 50 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar.
Baada ya kuundwa tume hiyo ilipewa miezi 18 ya kutekeleza jukumu la kukusanya maoni, kuyachambua na kutayarisha rasimu ya awali ili ijadiliwe na wananchi na kuandaa toleo hilo linalokabidhiwa kwa maraisi wiki ijayo.
Baada ya kuzunguka Bara na Visiwani Tume ilikusanya maoni kuyachambua na kutoa rasimu mpya iliyutoka Juni mwaka huu na kujadiliwa kwenye mabaraza ya katiba ili kuiboreshwa zaidi.
Miongoni mwa mambo yaliyoibuliwa na rasimu ya awali ni kuwepo kwa serikali tatu ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mapinduzi ya Zanzibar na Tanzania Bara.


Kadhalika ilizungumzia kuwepo kwa wagombea binafsi, kuondoa viti maalumu vya ubunge, kuweka ukomo wa ubunge na kuainisha mambo ya Muungano kuwa saba.

Bunge Maalumu
Kwa mujibu wa sheria ya mabadiliko ya katiba, baada ya kukabidhi rasimu hiyo ni kuitishwa Bunge Maalumu la Katiba.


Wajumbe wake ni wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano, Wawakilishi kutoka Baraza la wawakilishi Zanzibar na wajumbe 166 watakaochaguliwa na kutoka asasi za kiraia, vyama vya siasa, taasisi za elimu ya juu, wafanyakazi, wakulima na makundi maalumu.


Bunge hilo litaongozwa na Mwenyekiti ambaye ni kama Spika ambaye atakuwa na makamu na makatibu. Viongozi hao watachaguliwa kwa misingi ya Bara na Visiwani.



CHANZO: NIPASHE
 
jamani kesho ni kesho tutarajie nini warioba atakapowasilisha draft ya pili.maana draft ya kwanza magamba hawakuipenda na kufikia hatua ya kumtishia.
 
Dkt JK na DKt Shein kupokea rasimu ya katiba kesho uwanja wa Karimjee. Bila shaka jambo linalo vuta hisia ya wengi ni mapendekezo kuhusu mfumo wa muungano. Je tutegemee nini? Warioba kusuka au kunyowa?
 
Pamoja na vitisho vingi lakini tume imezingatia maoni ya wengi ya Serikali tatu.
 
Pamoja na vitisho vingi lakini tume imezingatia maoni ya wengi ya Serikali tatu.
And in fact, Serikali mbili na hata moja ni timely bomb, that will explode just with time...! USSR, pamoja na ukubwa wake, ilivunjika vipande vipande! Yugoslavia nayo imepotea kwenye ramani! Czechoslovakia imeingia kaburini nikiwa na akili zangu..miaka miwili iliyopita, South Sudan hiyoooo, imeachana na north! Scotland nao, si siri tena kwamba wanataka kuachana na UK...kwa kuangalia ukweli huu usiopingika, then I can easily conclude kwamba there's nothing special for Tanzania to last forever....NO GUARANTEE! Sooner or later, si ajabu kila mmoja akaenda kivyake!

Sasa basi, kwa wale wana-CCM wanaotaka serikali mbili sijui kama wanajiuliza what will happen in case muungano unavunjika wakati mfumo uliopo ni wa serikali mbili. Kwamba, assume 2015 CHADEMA wanachukua nchi! Sio siri, CHADEMA wakichukua nchi Muungano utakuwa kwenye majaribu makubwa. Sasa tuseme ndo hivyo, Rais wa Muungano ni CHADEMA na kule ZNZ Rais ni CCM or CUF. Je, hawa kweli wanaweza kufanya kazi pamoja?! I DOUBT! Na je, wakishindwa kufanya kazi pamoja, je Rais aliyopo wa Muungano ataendelea kuwa na sifa za kuwa Rais? Jibu HAPANA coz' kimsingi yeye alichaguliwa pia na wananchi wa Zanzibar hata kama alikuwa hakupata hata kura moja! Kutokana na hilo, automatically atapoteza sifa za kuwa Rais na matokeo yake Bara haitakuwa na Rais. Na wala nafasi yake haitawezekana kushikiwa japo kwa muda na Makamu wake, kwani obvious atakuwa ni Mzanzibari na hivyo hawezi kuongoza bara. Kama ndivyo, je CHADEMA watakubali kuachia kiti kirahisi namna hiyo wakati Katiba haisemi chochote? I DOUBT! Na wasipokubali, je CCM nao watakubali kuendelea kuongozwa na CHADEMA wakati wameshapoteza uhalali....I DOUBT AS WELL! Katiba inamtaja Speaker wa Bunge kushika kukaimu nafasi ya urais katika mazingira ambayo Rais hatakuwapo lakini ktk hili, kwenye UGOMVI WA MADARAKA, Speaker nae hatakuwa na sifa kwavile nae alichaguliwa na Wabunge wa Muungano! Labda Jaji Mkuu! Jaji wa sasa ni Mzanzibar, kwahiyo hana sifa za kuongoza bara unless awe amechaguliwa Jaji kutoka Bara kabla chokochoko hazijapamba moto!! Na kama hayo hayatakuwa yamefanyika, basi hakuna mwingine atakayekuwa na uwezo wa kumchagua Jaji Mkuu coz' nchi/bara haitakuwa na Rais...katika mvurugano huu ni kama naliona Jeshi likipata uhalali wa kuingia viunga vya Ikulu; God Forbid!!!..... Chonde chonde CCM, ikiwa rasimu mpya itakuja na pendekezo la serikali tatu, msitumie effort kubwa kuwataka watu wenu wazikatae...serikali mbili na hata moja ni bomu linalosubiria kuripuka bila kuguswa na yeyote!!!

c.c Mchambuzi, JokaKuu , Nguruvi3, chama, Ritz
 
Last edited by a moderator:
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom