OHA
Member
- Aug 20, 2013
- 34
- 42
Ndugu zangu watanzania poleni na majukumu na maumivu yaliyotawala miyoyoni mwenu takribani miaka 62 tangu nchi hii kupata uhuru.
Ndugu zangu msingi imara ndiyo huweka uimara wa nyumba inayojenda ukiboronga katika msingi nyumba hata uimarishe vipi nyufa za msingi lazima zionyeshe udhaifu wa nyumba.
Katiba bora ndiyo msingi bora katika kupeleka taifa lolote duniani katika matazamio wanayo yataka. Mpaka sasa kutokana na ubovu wa katiba iliyo tengenezwa na watu wa chache ndiyo inayo litafuna hili taifa.
Rai yangu kwa watanzania wenzangu tuungane na taasisi chama cha siasa chochote kile hususani kinacho taka kupeleka agenda yetu wananchi katika kupata katiba bora ya kutibu ugonjwa sugu unao tafuna hili taifa.
Hii kansa ya ufisadi na ubadhirifu wa mali za uma na miongo ya viongozi waliopita kama hatutaungana kwa pamoja na kusema sasa basi tutaendelea kuongozwa kifamilia kama nchi ilivyo sasa .
Nchi ikiongozwa na mfumo ule ule hakika mpaka tufike mafanikio tunayoyataka tutachelewa sana labda miaka 10,000 ijayo na hili sasa halitatufaa tena. Tuna madini kama tanzanite, nickel, uranium, zahabu, mbuga za wanyama milima, tunaweza kuchimba mafuta tuna makaa ya mawe, maziwa, mito bahari. Tuna aridhi yenye rutuba. Mambo kama shida ya maji, kutegemea kilimo cha mbua, shule hazina madawati, hatuna barabara bora mpaka leo tuna umaskini ulio kithirinni jambo la aibu sana.
Aridhi yetu amemilikishwa mtu aisimamie badala yetu ni kitu ambacho tunapaswa kukitafakari kwa kina na tutake katiba asubuhi mchana usiku kwanza kwa ari, na wivu mkubwa.
Tufike mahali kama taifa tulie mchagua apite na tuwe na uwezo wa kuwaondoa wabunge wetu katika majimbo tunayotoka kuondoa nafasi za uongozi ambazo ni za kisiasa na hazina tija katika mustakabali wa kulijenga taifa letu.
Watanzania wenzangu mwisho wa kuwa wajinga umeisha katiba sio ya wanasiasa katiba ni ya watanzania wote tunasomesha watoto tunauza aridhi tukijua mtoto atakuwa mkombozi wawadogo zake anabakia nyumbani hana mazingira sahihi ya kujiajiri alafu unaambiwa ajiajiri.
Narudia kusema tuitake katiba kwa mazingira sahihi yasiyo na fujo ili kutunza amani tuliyonayo na utawala waheshimu matakwa ya wananchi hii inchi ni ya kwetu wote hakuna ambaye ni yake peke yake keki ya taifa tugawane wote ili hata ukiimbwa wimbo wa taifa tuwe wanyenyekevu na kuwa na mapenzi thabiti kulingana na matunda tunayopata katika taifa letu.