Katiba mpya

Katiba mpya

Joined
Nov 22, 2013
Posts
13
Reaction score
1
Selikali isambaze katiba iliyopo ili wananchi wasome kilichomo, naona rasimu ndo inaonekana maeneo kadhaa lkn bado wananchi wengi hawaisomi na kuielewa
 

Attachments

Selikali isambaze katiba iliyopo ili wananchi wasome kilichomo, naona rasimu ndo inaonekana maeneo kadhaa lkn bado wananchi wengi hawaisomi na kuielewa
Wewe!!!!!Hivi hujui kuwa hao unaowatakia hizo nakala za Katiba na kutoa maoni ndiyo hao wanaendelea kuuwana kwa kugombea ardhi? Halafu umewahi kuona ukubwa wa kiatabu cha sheria ya ardhi? Kama kitabu hicho kimeshindwa kuwatosheleza waTz na bado wanaendelea kuuwana itakuwa kifungu kimoja au viwili unavyotaka kuweka katika katiba mpya? Mnatafuta Katiba ya ajabu sana ya kutaka mpaka Albino, kipofu, kiziwi kijana, mwanamme, mwanamke, mkulima, mfugaji, chotara, mchaga, mtindiga na mkurya etc watajwe ndani yake. Haki zote hizo za kiKatiba mtakazoweka mtakwenda kuzidai kwa Bush endapo zitavunjwa? Nauliza kama ni kwa Bush kwa sababu hizo zilizopo sasa hakuna mahali pa kuzidai isipokuwa kwa maPilato wetu hapa hapa. Philipo, tatizo siyo Katiba, tatizo ni Pilato anayesimamia Katiba na sheria hata zilizopo sasa hivi. Sheria ya ardhi ikivunjwa unakuta kuna FISADI, Kagasheki amekamata majangili wakati sheria zipo. Au unataka na haki za TEMBO ziingizwe kwenye Katiba yetu? Oyaaa! utasababisha nikutukane kukuita mbumbumbu kama mpaka leo hujajua tatizo siyo Katiba, tatizo ni MAJANGILI.Ngoja nikwambie mimi binafsi nimeshitaki Majaji kadhaa kwenye Kamati yao ya Maadili. Kamati hii ipo chini ya Jaji, mpaka leo tunaulizana tumbiri kweli unaweza kumshitaki kwa nyani? Sijajua hata karatasi zimekwenda wapi mika 3 sasa. Niliandika barua Ikulu kuulizia kwa kutuma kwa jina la JK mwenyewe lakini kuna ma miniJK mlangoni wanafungua wanasoma halafu wanaendesha biashara ngumu, utakutana na Jaji uliyemstaki Ikulu amekuwa MBOGO halafu wewe ndiyo unatafuta mahali pa kuhamia.Philipo usidhani Katiba mpya ni mwisho wa matatizo yako na yangu. Ni kiinimacho cha kutafutia ulaji na umaarufu. Ngoja utaona!
 
Back
Top Bottom