Mamshungulii
Senior Member
- May 3, 2023
- 175
- 88
Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ni katiba iliyotungwa mwaka 1977. Katiba hii inaielezea Tanzania kama nchi ya kidemokrasia, inayofuata misingi na haki za binadamu na siasa yake ni ya vyama vingi. Katiba ni sheria mama ya nchi inayowawezesha wananchi kujitambua kama taifa na ya kiutawala inayoelezea mgawanyo wa madaraka na majukumu ya vyombo mbalimbali vya dola.
Ibara ya 6 ya Katiba ya 1977 inatoa maana ya neno “Serikali” ambayo ni Serikali ya Jamhuri ya Muungano, Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Serikali za Mitaa na mtu yoyote anayefanya kazi kwa niaba ya serikali. Pamoja na kwamba Serikali-za-Mitaa zinatambulika na Katiba ya 1977 kama inavyoeleza muundo na kazi za serikali hii katika ibara ya 145 na 146 ya 1977, bado muundo na utekelezaji wa serikali hii si huru kama zilivyo serikali nyingine hususani Serikali Kuu na hatimaye kushindwa kufanya kazi kwa ufanisi zaidi.
Baada ya kusoma kwa makini katiba ya (1977) na Sheria za Serikali za Mitaa (1982 toleo la mwaka 2002) historia ya matendo ya watumishi wengi yamkini ni kwamba zipo changamoto na matatizo ya dhahiri yanayofifisha ufanisi wa Serikali-za-Mitaa.
Hii ni pamoja na utata wa kimuundo, kuingiliwa kimaamuzi, uwalakini kwenye mipango shirikishi na kutokuwa huru kwenye Mapato na Matumizi ya Rasilimali.
mapungufu yaliyomo katika katiba ya sasa yanayominya uhuru wa Serikali-za-Mitaa katika utendaji wa kazi zake na kutoa mapendekezo yatakayochangia uhitaji wa katiba mpya. mapungufu yaliyomo katika katiba ya sasa katika ngazi ya Serikali-za-Mitaa yanahitaji mabadiliko yapasa uwepo wa katiba mpya itakayokidhi uhuru na ufanisi wa Serikali-za-Mitaa. Uwepo wa serikali-za-mitaa Moja ya maaumzi ya muhimu sana katika kuandaa katiba, ni aina na muundo wa serikali. Muundo wa serikali au taifa lolote unatafsiriwa au kuoneshwa na mamlaka ya serikali na bunge ikiwemo uhusiano uliopo baina yao. Muundo huu ndiyo unaonyesha chombo kipi chenye mamlaka juu ya jambo fulani na rasilimali za taifa. Muundo wa Ugatuzi hutoa fursa ya kugawana madaraka baina ya Serikali Kuu na Serikali-za-Mitaa. Muundo wa Serikali iliyogatuliwa huwa na mamlaka zaidi yaliyo huru kuliko Serikali za Mitaa za kawaida. Kwa mantiki hiyo basi katika utendaji wa shughuli za kiserikali Tanzania ina serikali za ngazi mbili; yaani serikali kuu na serikali za mitaa. Kwa mujibu wa ibara ya 151(1), kifungu kidogo chakatiba ya 1977, kinasema Serikali za Mitaa maana yake ni vyombo vya kiserikali vilivyoundwa kwa mujibu wa ibara ya 145 ya Katiba ya 1977 kwa madhumuni ya kutekeleza madaraka ya umma.
Sheria ya Serikali-za-mitaa iliundwa mwaka 1982 na badae kuanza kutumika rasmi mwaka 1984 baada ya sheria ya madaraka mikoani ya mwaka 1972 kuonekana kuwa na ufanisi mdogo. Serikali-za-mitaa zinapata uhalali wake kupitia sura ya nane ya katiba 1977 Ibara ya 145(1) kifungu cha kwanza kinachosema kwamba kutakuwa na vyombo vya Serikali-za-Mitaa katika kila mkoa, wilaya, mji na kijiji, katika Jamhuri ya Muungano, ambavyo vitakuwa vya aina na majina yatakayowekwa na sheria iliyotungwa na bunge au baraza la wawakilishi. Madhumuni ya kuwepo kwa Serikali za Mitaa ni kupeleka madaraka kwa wananchi. Yamkini, viongozi wa Serikali za Mitaa hawawashirikishi wananchi katika mipango na shughuli za utekelezaji wa maendeleo katika sehemu zao. Ibara hii (146 (1)) iboreshwe kwa kuzitaka Serikali za Mitaa zifanye hivyo. Kwamba ni lazima viongozi wawashirikishe wananchi. Kiwepo kifungu cha wananchi kuwa na mamlaka ya kuwawajibisha watendaji haswa pale watendaji hawa wanaposhindwa kuwashirikisha wananchi. Kwahiyo vyombo vya Serikali za Mitaa vitakuwa na haki na mamlaka ya kushirikisha wananchi katika mipango na shughuli za utekelezaji wa maendeleo katika sehemu zao na nchini kote kwa jumla. Kwa mujibu wa Ibara ya 146(2) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, serikali za mitaa zitakuwa na majukumu ya fuatayo: Kutekeleza kazi za Serikali za Mitaa na kuimarisha demokrasia katika eneo lake, Kuhakikisha utekelezaji wa sheria na ulinzi wa wananchi na kuitumia demokrasia kuharakisha maendeleo ya wananchi.
Muundo wa serikali-za-mitaa Muundo umeainishwa katika sehemu ya tatu ya Sheria za Serikali za Mitaa ya 7 na 8 ya mwaka 1982. Sheria hizi zimeainisha kwamba, Serikali za Mitaa zinaundwa na Halmashauri ya Wilaya, Mamlaka za Miji na Vyombo vya Serikali za Vijiji. Katika muundo huu wa serikali za mitaa, baadhi ya vyombo vinavyounda serikali hii vinaongozwa na wenyeviti wanaochaguliwa miongoni mwa wanajamii wa eneo husika mfano Wenyeviti wa Vitongoji na Vijiji.
Ila ikumbukwe kwamba kwa sehemu kubwa Rais anayo madaraka ya kuteua watendaji wakuu katika Serikali Kuu. Mfano Rais ana mamlaka ya kuwateua Wakuu wa Wilaya, Wakuu wa Mikoa kama ilivyoainishwa katika ibara ya 61(2) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Makatibu Tawala wa Wilaya na Mikoa. Kwa mantiki hiyo basi, mamlaka haya makubwa aliyonayo Rais yanaminya uhuru wa Serikali za Mitaa katika utendaji wake wa kazi. Hii ni kwa sababu serikali hizi za mitaa kama ilivyo kwa watumishi wengine wa serikali,inafanya shughuli zake kwa niaba ya serikali na kwa amri na maagizo yatakayothibitishwa kwa namna itakavyoelezwa katika kanuni zilizowekwa na Rais kama ilivyoelezwa kwenye ibara ya 35(1) na (2) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Pia ibara ya 35(2) na 36(4) inampa Rais mamlaka ya kuteua na kuwawajibisha watendaji wa serikali. Kutokana na mamlaka aliyopewa Rais kwenye ibara ya 35(1), (2) na 36(4) kuna uwezekano mkubwa kwa viongozi ambao kimsingi ni wateule wa Rais kufanya kazi kwa malengo ya kukidhi matakwa ya Rais na si kwa ajili ya wananchi.
Ili kuepuka mapungufu hayo, Rais asiwe na mamlaka ya kuwateua na kuwawajibisha watendaji katika serikali za mitaa, badala yake wawe wanachaguliwa na wananchi katika mikoa na wilaya husika. Hii itasaidia kuondoa ukiritimba katika utendaji kazi wa serikali za mitaa na kuongeza ufanisi kwani watendaji katika serikali za mitaa watafanya kazi kwa moyo kutokana na uzoefu wa maeneo hayo na ufahamu wa matakwa ya wadau kwa kuwa ni makazi yao ya muda mrefu.
Serikali za mitaa ziwe na muundo wake wa uongozi na utendaji tofauti na serikali kuu.Ikiwezekana kuwepo na mwakilishi wa mtaa bungeni kuboresha mahusiano kikazi baina serikali kuu na serikali za mitaa. View attachment 2626407

Upvote
2