Katiba ni Mwafaka wa Kitaifa. Viongozi zungumzeni

Zitto

Former MP Kigoma Urban
Joined
Mar 2, 2007
Posts
1,562
Reaction score
10,888
Katiba ni Mwafaka wa Kitaifa. Viongozi zungumzeni
Kwa takribani wiki tatu sasa kumekuwa na sintofahamu kuhusu muswada wa sheria uliopitishwa na Bunge ili kufanya marekebisho ya sheria ya marekebisho ya Katiba ya mwaka 2011. Mjadala na upitishaji wa sheria hii uliweka rekodi ya pekee katika nchi yetu kwa vitendo vya kihuni kutokea Bungeni ambavyo nisingependa kuvirejea kutokana na aibu kubwa ambayo Bunge liliingia. Kiukweli kuna sintofahamu katika nchi kuhusu kuandikwa kwa Katiba mpya. Hii imechangiwa na kurushiana maneno miongoni mwa wanasiasa wa pande zote mbili, wanaopinga muswada ulivyo na wanaounga mkono muswada ulivyo. Masuala ya Tume imalize kazi yake lini, ushiriki wa Zanzibar na idadi ya wajumbe kutoka Zanzibar kwenye Bunge la Katiba, Wajumbe wa Bunge Maalumu wanapatikanaje na kadhalika ni masuala ambayo yanaweza kupatiwa mwafaka kwa viongozi kukaa na kuzungumza. Haya sio masuala ya kushindwa kujenga mwafaka labda kuwe na nia mbaya dhidi ya mchakato wa kuandika Katiba mpya. Katiba sio suala la kufanyia siasa. Katiba ni uhai wa Taifa.
Ni wazi kuna kundi kubwa ambalo halijitokezi waziwazi ambalo lingependa pasiwe na katiba mpya ya Wananchi. Kuna kundi lingine ambalo lingependa mchakato wa kuandika Katiba uendelee kwa miaka mingine zaidi ili kuweza kupata Katiba bora. Kuna kundi la Wabunge ambao kwa chinichini wanataka mchakato uendelee, uchaguzi uahirishwe mpaka mwaka 2017 na wao waendelee kuwa wabunge. Naamini watu hawa wanaota ndoto za mchana kwani hakuna mahusiano yeyote kati ya uchaguzi mkuu na kuandika katiba mpya. Kama Bunge hili la sasa na Serikali hii itashindwa kukamilisha zoezi hili, Bunge linalokuja na Serikali itakayoingia madarakani itaendelea nalo. Hivyo sio lazima kupata Katiba mpya kabla ya uchaguzi mkuu wa 2015. CHADEMA imependekeza kuwepo na marekebisho ya mpito kwenye Katiba ya sasa ili kuwezesha Tume huru ya Uchaguzi, masuala ya wagombea binafsi na kadhalika. Vyama vingine vya siasa vinaweza kuwa na mapendekezo yao ya mpito na hivyo kutoa nafasi ya kutosha kabisa wa kuandika Katiba makini.
Changamoto kubwa sana ya siasa za Tanzania ni kelele. Wanasiasa hatuzungumzi kwenye masuala yanayohusu uhai wa Taifa. Kila chama kinakuwa na misimamo yake na kuishikilia na hatimaye kujikuta tunapoteza fursa ya kuzungumza na kujadiliana kama Watanzania. Mwaka 2011 hali ilikuwa hivi hivi mpaka kundi la Wazee viongozi wastaafu walipoingilia kati na kupelekea wanasiasa kukaa na kuzungumza. Bahati mbaya sana viongozi wale ndio sasa wamepewa usukani wa kuandika Katiba kwa kuwa kwenye Tume. Hawawezi tena kufanya kazi ile ya kutafuta suluhu iliyopelekea Rais kuzungumza na viongozi wa vyama vyote vya siasa ikulu jijini Dar es Salaam.
Vyama vya Upinzani nchini sasa vimeungana kupinga muswada wa marekebisho ya Sheria ya Marekebisho ya Katiba ya mwaka 2011. Waziri wa Sheria na Katiba, Waziri wa Nchi ofisi ya Rais mahusiano na Uratibu, viongozi waandamizi wa CCM wote nao wameungana kuunga mkono muswada kama ulivyo. Badala ya kutafuta mwafaka, kumekuwa na kurushiana maneno ya kejeli na kadhalika. Taifa halijengwi namna hii. Taifa linajengwa kwa mwafaka na Katiba ni moja ya nyenzo wa Mwafaka wa Taifa. Niliwahi kuandika huko nyuma kuwa Katiba haiandikwi barabarani bali huandikwa mezani kwa watu kukaa na kukubaliana masuala ya Taifa dhidi ya maslahi ya kivyama ya wanasiasa.
Hakuna kilichoharibika. Bado tunayo nafasi kama Taifa kukaa na kukubaliana. Kwa hali ya sasa nafasi hii ipo mikononi mwa Mkuu wa Nchi, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Rais ana wajibu wa kikatiba wa kuhakikisha umoja wa kitaifa unaendelea kuongoza mchakato huu wa katiba ya nchi yetu. Hata hivyo ni vizuri kutahadharisha kuwa sio sahihi kwa wanasiasa wa pande zote kujaribu kumlazimisha Rais kuridhia ama kutoridhia sheria hiyo. Si sawa kisiasa kwa wanasiasa wa upinzani kujaribu kumlazimisha Rais ambaye pia ni Mwenyekiti wa chama chenye wabunge wengi bungeni kwenda tofauti na wabunge wake na wakati huohuo ni utovu wa nidhamu kwa Waziri wa Sheria kujaribu kumshauri hadharani Rais wake kuridhia sheria hiyo kwani ni kinyume cha misingi ya uongozi na pia kinatafsirika kama kumshurutisha (blackmail) Rais wake.
Kutosaini muswada huu kunaweza kuleta mgongano kati ya Wabunge wa CCM na Rais. Hata hivyo Rais lazima aweze kushawishi chama chake kwamba umoja wa kitaifa ni muhimu ziadi kuliko maslahi ya kisiasa ya chama chao. Pia kikatiba Rais anasaini miswada kuwa sheria akiwa Mkuu wa Nchi na sio Mkuu wa Serikali ya Jamhuri. Akiwa Mkuu wa Nchi maslahi mapana ni kuweka mwafaka wa pamoja miongoni mwa wananchi. Rais Jakaya Kikwete anapaswa kutumia mamlaka yake kama Mkuu wa Nchi kuiweka nchi pamoja kwa kuurejesha muswada bungeni ili uweze kujadiliwa upya na wadau wote na kupitishwa tena na Bunge. Ibara ya 97 ya Katiba ya sasa imeweka masharti ya utaratibu wa kutunga sheria na iwapo Rais ataurudisha muswada huu Bungeni pamoja na maelezo ya hatua hii, upitishwaji wake utahitaji theluthi mbili ya wabunge wote. Hii itakuwa hatua muhimu sana katika historia ya demokrasia yetu. Rais afuate ushauri huu kwani una manufaa makubwa.
Hata hivyo, ni lazima pawepo na mazungumzo miongoni mwa wanasiasa na makundi ya kijamii kuhusu Katiba. Katiba nzuri itapatikana pale tu ambapo mazingira ya kisiasa yanaonyesha nia njema kwa pande zote kisiasa. Kukwepa kuangaliana machoni na kuzungumza tofauti zetu za kimitazamo ni hatari zaidi. Juzi ngumi zimerushwa Bungeni. Kesho zitakua mitaani na vijijini kwetu. Tunataka kujenga Taifa la namna hiyo?
 
maneno haya unapaswa kuwaambia mbowe lipumba na mbatia kabla ya kuwambia watu wengine.

wewe ni naibu katibu mkuu wa chama kinachofanya fujo na kudai katiba kwenye mikutano ya hadhara.

kama naibu katibu mkuu umefanya jitihada gani za kuongea na mbowe na wanasiasa wengine wenye vichwa hewa.

kama hujaongea na chama chako hasa mwenyekiti na katibu mkuu wako ukawambia wanachofanya utoto nitakuona kama mnafiki tu unayechezea akili za watu.
 
Nadhani akili kubwa na ndogo kila siku zinazidi kuwa wazi.... Hakika unaweza kuwahadaa watu siku zote lakini ni vigumu sana kuficha asili yako mara zote. Nimekuelewa, nimekupata...... But what is your position in this matter ukiwa Makamu Kiongozi wa Kambi ya Upinzani Bungeni, vile vile ukiwa Naibu Katibu Mkuu wa Chadema...Tumewasikia akina mtatiro, na leo nimepata what you are thinking.........Akili yangu ndogo kweli haina uwezo wa kuongoza kubwa..... Inyanka kubwigwa ibwigwa na maso gutukura............................
 
Zitto Zitto, hebu kwanza rekebisha habari yako...Weka paragraph pliz
 
Last edited by a moderator:

Mkuu wangu Zitto naheshimu sana mawazo yangu na yako pia na nakuheshimu kama kiongozi wangu ila ninataka nitofautiane na wewe na watz wengine kwenye suala la NGUMI bungeni. NGUMI kwa maslahi ya nchi sawa sawa sijui watz tunamatatizo gani mataifa makubwa tu wanatwangana sembuse sisi omba omba? Hebu tazama juzi juzi tu hapa Japan wametwangana walipokuwa wanajadili sheria ya kudhibiti mafukushima yao yanayovuja, India wlitwngana, Kenya, Pakistan juzi tu baada ya filamu ya bunge letu Nigeria walitwngana. Sasa hofu ya ngumi iko wapi? Watu mmekuwa waoga wa ngumi kwa maslahi zaidi ya tunavyoogopa HIV. Mbona hatuogopi watz wanaokufa kwa kukosa matibabu? vp watu wa North Mara wanaokunywa maji ya sumu? Mbona hamuogopi? NGUMI BUNGENI KWA MASLAHI YA UMMA TUACHANE NA MAWAZO YA KICCM CCM KUTISHA WATU HATA KWENYE MAMBO YA MSINGI. Tafakari!!! Chukua Hatua!!!!
 
  • Thanks
Reactions: BAK

Mkuu ZZK,nimefarijika sana kukuona kipande hii. Nimekusoma sasa najaribu kukuelewa
Pasco
 
Hivi ni wewe kweli Zitto, sijakuelewa uko upande gani maana uko katikati ya mstari hebu sogeza kabisa mguu tuelewe uko upande gani. Lugha uliyotumia ni ya kubembeleza sana, unabembeleza nini wakati unaujua ukweli, najua unajua ni wapi? wanaotetea masilahi ya Taifa na wapi wanaotetea masilahi yao.
 
Mkuu Zitto heshima sana.

1. Hiyo sheria imepitishwa na wabunge wa CCM 126 wengine walisepa; kwa maana hiyo Rais atakuwa kituko kusaini sheria isiyokidhi matakwa ya Bunge.

2. Kingereza wana sema tumia "COMMON SENSE" Ndani ya CCM Sense is not common mapAka akili zao hazifikirii taifa zinafikiria CCM isiwafie mikononi wakaweka historia.

3. CCM ni mabingwa wa kutibua michakato kwa kutumia majanga. Wanatafuta janga ili wapate fursa na muda kujipanga. Si watu wakukaa nao mezani.

4. Bunge linatoa fursa nzuri kuweka umoja wa kitaifa wewe unakiri hii sheria imepitishwa kiana yake (mimi natafsiri kihuni) ukowapi ukomavu wa wabunge waliopitisha sheria hii kimtazamo wa kitaifa? Majanga.

5. Muungano wa vyama na asasi CCM waliupanga na waliutegemea kwenye hili. Kilichowastua ni kuungwa mkono na wananchi na fursa ya magwiji kutoa shule iliyoshiba kuhusu uhuni wa CCM.

6. Siamini ukuu wa nchi wa dhaifu wala urais wake, namuona yeye ni mwana mtandao fulani nyuma ya pazia aliyekuwa na "mission" ambayo imejikanganya mahali fulani na anataka kuilinda. Hana tofauti na akina Uhuru Kenyata. Ushahidi ni Werema kutumia wadhifa aliopewa kuwatetea wahalifu the Hague kama msimamo wa Tanzania. Hapa Katiba haitapatikana hata kwa mazungumzo. Mfano wa leo ni mikataba yote ya madini inayowekwa sahihi sasa itakuwa wazi sasa ila iliyotanguliwa itabaki kuwa siri. Wahalifu akiwepo dhaifu wako wanataka katiba ya kuficha uovu wao. HAITAKUBARIKA.

7. Muungano wa vyama unatoa elimu tu, mimi najua dhaifu ataweka saini kwa sababu sheria ina manufaa kweke na hajali. Ni kutokana na elimu inayotolewa wananchi wanakuwa "empowered" kuchukuwa wajibu wao na vingozi wa vyama kiusahihi watakuwa wametimiza wajibu wao.

8. Machafuko baada ya hapo yatafanywa na CCM na watawala na si wananchi. Uzuri wananchi hawataingizwa mkenge wakiwa hawajui baada ya kuelimishwa.

9. Kinachotugawanya sasa hivi si mchakato wa Katiba, TUNAGAWANYWA NA KITU KIMOJA TU "SURVIVAL YA CCM" baada ya kujihukumu yenyewe.

10. Ungetoa ushauri ambao hata mtoto mdogo au mzee sana angekuelewa. Mtoto anajua right and wrong, mzee anajua dhamira njema na mbaya.

Umefanya vyema sana kutoa mawazo yako ila jiunge na DHAMIRA YA NCHI ISYOGAWANYIKA KWA HILA.
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Swali zuri sana hili Mkuu lakini sijui kama utapata jibu lake. Anauma na kupuliza hapo hapo!!! unashindwa kumuelewa kasimama kipande ipi!!!!

Nadhani akili kubwa na ndogo kila siku zinazidi kuwa wazi.... Hakika unaweza kuwahadaa watu siku zote lakini ni vigumu sana kuficha asili yako mara zote. Nimekuelewa, nimekupata...... But what is your position in this matter ukiwa Makamu Kiongozi wa Kambi ya Upinzani Bungeni, vile vile ukiwa Naibu Katibu Mkuu wa Chadema...Tumewasikia akina mtatiro, na leo nimepata what you are thinking.........Akili yangu ndogo kweli haina uwezo wa kuongoza kubwa..... Inyanka kubwigwa ibwigwa na maso gutukura............................
 
Ahsante sana Mkuu chikutentema.

Mkuu wangu Zitto naheshimu sana mawazo yangu na yako pia na nakuheshimu kama kiongozi wangu ila ninataka nitofautiane na wewe na watz wengine kwenye suala la NGUMI bungeni. NGUMI kwa maslahi ya nchi sawa sawa sijui watz tunamatatizo gani mataifa makubwa tu wanatwangana sembuse sisi omba omba? Hebu tazama juzi juzi tu hapa Japan wametwangana walipokuwa wanajadili sheria ya kudhibiti mafukushima yao yanayovuja, India wlitwngana, Kenya, Pakistan juzi tu baada ya filamu ya bunge letu Nigeria walitwngana. Sasa hofu ya ngumi iko wapi? Watu mmekuwa waoga wa ngumi kwa maslahi zaidi ya tunavyoogopa HIV. Mbona hatuogopi watz wanaokufa kwa kukosa matibabu? vp watu wa North Mara wanaokunywa maji ya sumu? Mbona hamuogopi? NGUMI BUNGENI KWA MASLAHI YA UMMA TUACHANE NA MAWAZO YA KICCM CCM KUTISHA WATU HATA KWENYE MAMBO YA MSINGI. Tafakari!!! Chukua Hatua!!!!
 
Last edited by a moderator:
Hivi ni wewe kweli Zitto, sijakuelewa uko upande gani maana uko katikati ya mstari hebu sogeza kabisa mguu tuelewe uko upande gani. Lugha uliyotumia ni ya kubembeleza sana, unabembeleza nini wakati unaujua ukweli, najua unajua ni wapi? wanaotetea masilahi ya Taifa na wapi wanaotetea masilahi yao.
Mkuu huyu bao hujamjuaga tu atakupa shida sana, wengine siku hizi hatupi shida kabisa kijana unapokuwa mnafiki ukizeeka ni Mchawi tu
 
Katiba ni Mwafaka wa Kitaifa. Viongozi zungumzeni
Kwa takribani wiki tatu sasa kumekuwa na sintofahamu kuhusu muswada wa sheria uliopitishwa na Bunge ili kufanya marekebisho ya sheria ya marekebisho ya Katiba ya mwaka 2011. Mjadala na upitishaji wa sheria hii uliweka rekodi ya pekee katika nchi yetu kwa vitendo vya kihuni kutokea Bungeni ambavyo nisingependa kuvirejea kutokana na aibu kubwa ambayo Bunge liliingia. Kiukweli kuna sintofahamu katika nchi kuhusu kuandikwa kwa Katiba mpya. Hii imechangiwa na kurushiana maneno miongoni mwa wanasiasa wa pande zote mbili, wanaopinga muswada ulivyo na wanaounga mkono muswada ulivyo. Masuala ya Tume imalize kazi yake lini, ushiriki wa Zanzibar na idadi ya wajumbe kutoka Zanzibar kwenye Bunge la Katiba, Wajumbe wa Bunge Maalumu wanapatikanaje na kadhalika ni masuala ambayo yanaweza kupatiwa mwafaka kwa viongozi kukaa na kuzungumza. Haya sio masuala ya kushindwa kujenga mwafaka labda kuwe na nia mbaya dhidi ya mchakato wa kuandika Katiba mpya. Katiba sio suala la kufanyia siasa. Katiba ni uhai wa Taifa.
Ni wazi kuna kundi kubwa ambalo halijitokezi waziwazi ambalo lingependa pasiwe na katiba mpya ya Wananchi. Kuna kundi lingine ambalo lingependa mchakato wa kuandika Katiba uendelee kwa miaka mingine zaidi ili kuweza kupata Katiba bora. Kuna kundi la Wabunge ambao kwa chinichini wanataka mchakato uendelee, uchaguzi uahirishwe mpaka mwaka 2017 na wao waendelee kuwa wabunge. Naamini watu hawa wanaota ndoto za mchana kwani hakuna mahusiano yeyote kati ya uchaguzi mkuu na kuandika katiba mpya. Kama Bunge hili la sasa na Serikali hii itashindwa kukamilisha zoezi hili, Bunge linalokuja na Serikali itakayoingia madarakani itaendelea nalo. Hivyo sio lazima kupata Katiba mpya kabla ya uchaguzi mkuu wa 2015. CHADEMA imependekeza kuwepo na marekebisho ya mpito kwenye Katiba ya sasa ili kuwezesha Tume huru ya Uchaguzi, masuala ya wagombea binafsi na kadhalika. Vyama vingine vya siasa vinaweza kuwa na mapendekezo yao ya mpito na hivyo kutoa nafasi ya kutosha kabisa wa kuandika Katiba makini.
Changamoto kubwa sana ya siasa za Tanzania ni kelele. Wanasiasa hatuzungumzi kwenye masuala yanayohusu uhai wa Taifa. Kila chama kinakuwa na misimamo yake na kuishikilia na hatimaye kujikuta tunapoteza fursa ya kuzungumza na kujadiliana kama Watanzania. Mwaka 2011 hali ilikuwa hivi hivi mpaka kundi la Wazee viongozi wastaafu walipoingilia kati na kupelekea wanasiasa kukaa na kuzungumza. Bahati mbaya sana viongozi wale ndio sasa wamepewa usukani wa kuandika Katiba kwa kuwa kwenye Tume. Hawawezi tena kufanya kazi ile ya kutafuta suluhu iliyopelekea Rais kuzungumza na viongozi wa vyama vyote vya siasa ikulu jijini Dar es Salaam.
Vyama vya Upinzani nchini sasa vimeungana kupinga muswada wa marekebisho ya Sheria ya Marekebisho ya Katiba ya mwaka 2011. Waziri wa Sheria na Katiba, Waziri wa Nchi ofisi ya Rais mahusiano na Uratibu, viongozi waandamizi wa CCM wote nao wameungana kuunga mkono muswada kama ulivyo. Badala ya kutafuta mwafaka, kumekuwa na kurushiana maneno ya kejeli na kadhalika. Taifa halijengwi namna hii. Taifa linajengwa kwa mwafaka na Katiba ni moja ya nyenzo wa Mwafaka wa Taifa. Niliwahi kuandika huko nyuma kuwa Katiba haiandikwi barabarani bali huandikwa mezani kwa watu kukaa na kukubaliana masuala ya Taifa dhidi ya maslahi ya kivyama ya wanasiasa.
Hakuna kilichoharibika. Bado tunayo nafasi kama Taifa kukaa na kukubaliana. Kwa hali ya sasa nafasi hii ipo mikononi mwa Mkuu wa Nchi, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Rais ana wajibu wa kikatiba wa kuhakikisha umoja wa kitaifa unaendelea kuongoza mchakato huu wa katiba ya nchi yetu. Hata hivyo ni vizuri kutahadharisha kuwa sio sahihi kwa wanasiasa wa pande zote kujaribu kumlazimisha Rais kuridhia ama kutoridhia sheria hiyo. Si sawa kisiasa kwa wanasiasa wa upinzani kujaribu kumlazimisha Rais ambaye pia ni Mwenyekiti wa chama chenye wabunge wengi bungeni kwenda tofauti na wabunge wake na wakati huohuo ni utovu wa nidhamu kwa Waziri wa Sheria kujaribu kumshauri hadharani Rais wake kuridhia sheria hiyo kwani ni kinyume cha misingi ya uongozi na pia kinatafsirika kama kumshurutisha (blackmail) Rais wake.
Kutosaini muswada huu kunaweza kuleta mgongano kati ya Wabunge wa CCM na Rais. Hata hivyo Rais lazima aweze kushawishi chama chake kwamba umoja wa kitaifa ni muhimu ziadi kuliko maslahi ya kisiasa ya chama chao. Pia kikatiba Rais anasaini miswada kuwa sheria akiwa Mkuu wa Nchi na sio Mkuu wa Serikali ya Jamhuri. Akiwa Mkuu wa Nchi maslahi mapana ni kuweka mwafaka wa pamoja miongoni mwa wananchi. Rais Jakaya Kikwete anapaswa kutumia mamlaka yake kama Mkuu wa Nchi kuiweka nchi pamoja kwa kuurejesha muswada bungeni ili uweze kujadiliwa upya na wadau wote na kupitishwa tena na Bunge. Ibara ya 97 ya Katiba ya sasa imeweka masharti ya utaratibu wa kutunga sheria na iwapo Rais ataurudisha muswada huu Bungeni pamoja na maelezo ya hatua hii, upitishwaji wake utahitaji theluthi mbili ya wabunge wote. Hii itakuwa hatua muhimu sana katika historia ya demokrasia yetu. Rais afuate ushauri huu kwani una manufaa makubwa.
Hata hivyo, ni lazima pawepo na mazungumzo miongoni mwa wanasiasa na makundi ya kijamii kuhusu Katiba. Katiba nzuri itapatikana pale tu ambapo mazingira ya kisiasa yanaonyesha nia njema kwa pande zote kisiasa. Kukwepa kuangaliana machoni na kuzungumza tofauti zetu za kimitazamo ni hatari zaidi. Juzi ngumi zimerushwa Bungeni. Kesho zitakua mitaani na vijijini kwetu. Tunataka kujenga Taifa la namna hiyo?

Tafadhali Mkuu popote ulipo njoo hapa jamvini kama anavyofanyaga mnyika tuwekane sawa mi ninamengi sana na wewe mkuu wangu plz plz !!
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Magwanda yanaposhindana na magwanda.

Uchaguzi wa magwanda lini?
 
Gamba mnalivua lini? Au mafisadi, wauza unga, majangili na magaidi ndio wameshakumbatia utamu ndani ya chama chenu?

Babu anasema hakuna uchaguzi mpaka chama kiwe imara, halafu yeye anakwenda na mchumba kukiimarisha chama Washington, Jerusalem, Vatican ...

Magwanda mnachekesha kweli-kweli. Misukule ya uhakika.
 
Mkuu wangu Zitto naheshimu sana mawazo yangu na yako pia na nakuheshimu kama kiongozi wangu ila ninataka nitofautiane na wewe na watz wengine kwenye suala la NGUMI bungeni. NGUMI kwa maslahi ya nchi sawa sawa sijui watz tunamatatizo gani mataifa makubwa tu wanatwangana sembuse sisi omba omba? Hebu tazama juzi juzi tu hapa Japan wametwangana walipokuwa wanajadili sheria ya kudhibiti mafukushima yao yanayovuja, India wlitwngana, Kenya, Pakistan juzi tu baada ya filamu ya bunge letu Nigeria walitwngana. Sasa hofu ya ngumi iko wapi? Watu mmekuwa waoga wa ngumi kwa maslahi zaidi ya tunavyoogopa HIV. Mbona hatuogopi watz wanaokufa kwa kukosa matibabu? vp watu wa North Mara wanaokunywa maji ya sumu? Mbona hamuogopi? NGUMI BUNGENI KWA MASLAHI YA UMMA TUACHANE NA MAWAZO YA KICCM CCM KUTISHA WATU HATA KWENYE MAMBO YA MSINGI. Tafakari!!! Chukua Hatua!!!!
Zitto , katika mambo mengine na sababu zilizo nyuma ya pazia ya mambo hayo, mpenda haki hawezi kuwa neutral. Suala la katiba, hoja zikishindikana, hata ngumi ni halali. Sasa hivi rasilimali za Watanzania kama ardhi, madini, gesi n.k. zinagawiwa kwa wageni na wazawa wanashindwa kujitetea kwa sababu ya katiba mbovu. Mwisho wa siku tunaambulia kuambiwa ni sababu ya mikataba mibovu. Hata wewe umeshindwa kuendeleza hoja ya fedha zilizofichwa nje ya nchi kwa sababu ya ubovu wa Katiba iliyopo. Hili haliwezi kuendelea. Mzengwe unaundwa ili kuwezesha CCM kushinikiza katiba ya zamani na hapo bado wenye akili wanataka kuwa neutral. Haiwezekani. Haki inapiganiwa na wala haiombwi kwa vile mafisadi kamwe hawatakubali kuiachia kirahisi! Si dhani kuwa hapa kuna muafaka. Mswada urudishwe bungeni na urekebishwe tu. Nadhani JK hatausaini!
 
Kiukweli watu kutumia shida zetu kuendeleza maslahi yao, Mona ukimwi unatumaliza watu hatutumii busara kuuepuka(starehe), Elimu yetu inadidimia kila siku mbona hatujasikia hata busara ya hawa wanaotaka busara leo, mama dada n awake zetu wanapalamiwa(bakwa) HUKO MTWARA na majeshi kama kuku hawa mashetani hawaioni hyo busara yao,ila leo kwenye kiini cha ulaji(KATIBA) ndio mtu anaibuka shimoni na busara ambayo hajawahi kuwa nayo hata siku moja. Sio siri ninahasira na kauli za kipumbavu kama hizi...Eti busara!!!! SHIT!!!!!!!! I SAY OUR DAY WILL COME, WHEN ALMIGHTY GOD WILL STOP THE SUN, TO LET US IN LIGHT TILL WE WIN THE BATTLE LIKE IN THE DAYS OF JOSHUA
 
Back
Top Bottom