Katiba ni takwa kwa watu wote

Katiba ni takwa kwa watu wote

OHA

Member
Joined
Aug 20, 2013
Posts
34
Reaction score
42
Katiba ni takwa kwa watu wote
Bila kuwa na katiba hakuna tafsiri sahihi ya muongozo wa nchi. Ukitaka uweke utaratibu wa uwajibikaji lazima tuwe na katiba dhabiti inayobeba mwelekeo wa wananchi na yenye kuwa na usawa.

Kwanini katiba inampa kinga rais, spika, waziri mku na mwanasheria mkuu maana yake katiba inaweza kuchezewa ili uwajibishwaji usiwepo.

Ili kujenga nchi imara na uwajibikaji kwa watu wote katiba ya mzee warioba imejieleza vizuri na inawapa wananchi malaka ya kumuwajibisha muwakilishi yani Mbunge kabla hata ya kumaliza muda wake.

Pia anapo tokea mtu kutoa matamko yasio endana na kikatiba inapaswa awajibishwe kisheria iwe baada au kabla.
Tuondoe teuzi ambazo zinalenga kuretaini wawajibikaji ambao watatetea tawala zilizo madarakani.

Rasimu ilioandaliwa chini ya uongozi wa warioba natumaini mama akiitukia itatusaidia kuweza kufikia uchumi ambao mama anautizamia na haitakuwa na makando kando yanayo leta ukakasi.

Katiba mpya ndiyo dira na nyenzo ya kutufikisha uchumi ulio dhabiti na wabunge wawapo bungeni watambue hawaendi kutetea chama wanaenda kutetea maslahi ya nchi.

Tunataka ufike mahali tuone hela tunazo lipa wabunge zinaendana na utendaji na uwajibikaji kuliko waende kupiga makofi bure bila kutusaidia wananchi tulicho watuma
 
Kuna mengi tu ya kurebisha. Hebu fikiria, Kaijage, Mahera na Jamana Printers wakishamtangaza mgombea wa CCM eti ni mshindi wa urais, hakuna mtu anayeweza kupinga mahakamani! Kuna siku Kaijage atamtangaza mke wa Mahera ambaye hakugombea urais kuwa kashinda uchaguzi na atakuwa Rais kwa katiba yetu mbovu.
 
Anayeogopa katiba yenye kutoa nafasi sawa kwa Watanzania wote ni mwizi/jambazi tu. Anafaidika na ujambazi na ataka aendelee nao. Na ndio maana wanaitwa chama cha majambazi.
 
Kuna mengi tu ya kurebisha. Hebu fikiria, Kaijage, Mahera na Jamana Printers wakishamtangaza mgombea wa CCM eti ni mshindi wa urais, hakuna mtu anayeweza kupinga mahakamani! Kuna siku Kaijage atamtangaza mke wa Mahera ambaye hakugombea urais kuwa kashinda uchaguzi na atakuwa Rais kwa katiba yetu mbovu.
Tuna haja hata hizi tume ziwekwe na wananchi na rais asiteue watu ambao watakuwa muhimili wa kumlinda ndiyo maana tunataka rasimu ya warioba wakurugenzi, wakuu wa mikoa wilaya wako kisiasa tu ila mtendaji ni mbunge. Na ifike mahali isi nafasi ziwe ili kuweka uwajibikaji pindi itakapo bainika kunaubadhilifu wa kimadaraka.

Kujenga uwajibikaji na kuwaweka watu kufahamu wanalitumikia taifa sio mtu inasikitisha sana kwa kutokuwa na hofu na uchungu wa taifa letu.

Tukiwa na katiba madhubuti kero za ufisadi matumizi mabaya ya madaraka , kero ya maji, madawati tunaweza kuimaliza kwa kipindi kifupi sana
 
Back
Top Bottom