Katiba pendekezwa ndio suluhisho la kudumu kwa kero na matatizo sugu ya muungano

Katiba pendekezwa ndio suluhisho la kudumu kwa kero na matatizo sugu ya muungano

singidadodoma

JF-Expert Member
Joined
Nov 11, 2013
Posts
4,394
Reaction score
1,536
Katiba Inayopendekezwa pia inatoa fursa ya kuunda tume ya usimamizi wa uratibu wa mambo ya Muungano, chombo kitakachoshughulikia moja kwa moja mambo ya Muungano na malalamiko yake wakati yanapotokea kupatiwa ufumbuzi moja kwa moja kwa wakati muafaka.

Sura ya tisa ya katiba kifungu 127 hadi 128 (1) tume hiyo itakuwa na majukumu ya kuratibu ushirikiano wa kisera katika mambo ya Muungano kisheria na kikatiba. Aidha Katiba inaweka utaratibu bora na endelevu kushauriana na kushirikiana pamoja na utaratibu wa kusuluhisha na kutatua migogoro baina ya pande mbili za Muungano.

Kifungu hicho sasa kitahakikisha kero za Muungano zinazoweza kujitokeza zitapatiwa ufumbuzi wa haraka kwa sababu itaundwa Tume ya kufanya kazi hizo pamoja na Mwenyekiti wake na watumishi. "Huo ndiyo ubora wa Katiba Inayopendekezwa, yale mambo yote ambayo tuliona yanaleta usumbufu mara kwa mara na kikwazo katika Muungano wetu sasa tumeyapatiwa ufumbuzi na kuweka mikakati ya kudumu juu ya njia za kuyasuluhuhisha," Vuai anaeleza.

Wapinzani wamekuwa wakipotosha kwa makusudi licha ya kufahamu ukweli ni juu ya mamlaka ya Rais ya uteuzi wa wakuu wa mikoa kutoka Zanzibar, ambapo wanadai kwamba Rais wa Zanzibar katika Katiba Inayopendekezwa sasa hana uwezo tena wa kuteua viongozi hao.

Katika Katiba Inayopendekezwa ibara 123 (1) inasema kutakuwa na wakuu wa mikoa wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania bila ya kuathiri ibara ndogo ya 3, watakuwa viongozi katika Serikali ya Muungano. Aidha anasema kifungu cha katiba cha 2 hadi 3 wakuu wa mikoa watateuliwa na Rais baada ya kushauriana na Waziri Mkuu na wale wakuu wa mikoa wa Zanzibar watateuliwa na Rais wa Zanzibar.

Ajabu kwa makusudi kabisa Cuf, wamekuwa wakipotosha umma eti yakuwa Rais wa Zanzibar hana uwezo wa kuteuwa wakuu wa mikoa au sheha, sasa anaweza kuteuliwa kutoka Sengerema, Huo ni upotoshaji wa makusudi unaofanywa na CUF kwa ajili ya kuwashawishi wananchi waikataye Katiba Inayopendekezwa ambayo imeweka ufafanuzi wa wazi katika kila eneo.
 
Katiba Inayopendekezwa pia inatoa fursa ya kuunda tume ya usimamizi wa uratibu wa mambo ya Muungano, chombo kitakachoshughulikia moja kwa moja mambo ya Muungano na malalamiko yake wakati yanapotokea kupatiwa ufumbuzi moja kwa moja kwa wakati muafaka.

Sura ya tisa ya katiba kifungu 127 hadi 128 (1) tume hiyo itakuwa na majukumu ya kuratibu ushirikiano wa kisera katika mambo ya Muungano kisheria na kikatiba. Aidha Katiba inaweka utaratibu bora na endelevu kushauriana na kushirikiana pamoja na utaratibu wa kusuluhisha na kutatua migogoro baina ya pande mbili za Muungano.

Kifungu hicho sasa kitahakikisha kero za Muungano zinazoweza kujitokeza zitapatiwa ufumbuzi wa haraka kwa sababu itaundwa Tume ya kufanya kazi hizo pamoja na Mwenyekiti wake na watumishi. “Huo ndiyo ubora wa Katiba Inayopendekezwa, yale mambo yote ambayo tuliona yanaleta usumbufu mara kwa mara na kikwazo katika Muungano wetu sasa tumeyapatiwa ufumbuzi na kuweka mikakati ya kudumu juu ya njia za kuyasuluhuhisha,” Vuai anaeleza.

Eneo jingine ambalo wapinzani wamekuwa wakipotosha kwa makusudi licha ya kufahamu ukweli ni juu ya mamlaka ya Rais ya uteuzi wa wakuu wa mikoa kutoka Zanzibar, ambapo wanadai kwamba Rais wa Zanzibar katika Katiba Inayopendekezwa sasa hana uwezo tena wa kuteua viongozi hao.

Katika Katiba Inayopendekezwa ibara 123 (1) inasema kutakuwa na wakuu wa mikoa wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania bila ya kuathiri ibara ndogo ya 3, watakuwa viongozi katika Serikali ya Muungano. Aidha anasema kifungu cha katiba cha 2 hadi 3 wakuu wa mikoa watateuliwa na Rais baada ya kushauriana na Waziri Mkuu na wale wakuu wa mikoa wa Zanzibar watateuliwa na Rais wa Zanzibar.

Ajabu kwa makusudi wamekuwa wakipotosha umma eti yakuwa Rais wa Zanzibar hana uwezo wa kuteuwa wakuu wa mikoa au sheha, sasa anaweza kuteuliwa kutoka Sengerema, Huo ni upotoshaji wa makusudi unaofanywa na CUF kwa ajili ya kuwashawishi wananchi waikataye Katiba Inayopendekezwa ambayo imeweka ufafanuzi wa wazi katika kila eneo.

watanzania wote bara na visiwani kwa umoja wetu tuipigie kura ya ndio katiba pendekezwa kwa mustakabali mwema wa muungano wetu na vizazi vyetu vijavyo kama sisi tulivyoachiwa na waasisi wetu,
 
Hapo hapo! MkulimaWakiteto, nipe ramani. Kumbe ni nzuri hivyo? Tuiunge mkono hiyo Katiba Inayopendekezwa kwa manufaa yetu sote Watanzania.
 
Hapa imekaa njema sana!lazima mtawala awe na watu wa kumsaidia katika mikoa na wilaya!sasa kuna watu eti wanataka kutupa jukumu hilo sisi wananchi wapi na wapi si tutawamaliza tunamuweka asubuhi afu usiku tunawatoa kwa chuki na siasa zetu za UKAWA ni balaa!
 
Back
Top Bottom