Kweli kabisa Sentino,ukisogea mbele tu hapo Sura ya Saba, ndani ya katiba inayopendekezwa ,utakutana na MUUNDO WA JAMHURI YA MUUNGANO, ibara ya ya 73,inasema Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania itakuwa na muundo wa serikali mbili ambazo a) Serikali ya Jamhuri ya Muungano na b) Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar na hapo ibara ya 74 ni utekelezaji wa shughuli za Mamlaka ya nchi.
Asante Sentino umenifanya na mie kuisoma katiba Pendekezwa, kumbe ukituliza kichwa bwana mambo yanaeleweka kuliko kusimliwa na wanasiasa.