Sijui wewe, lakini mimi nakerwa sana na hili wajumbe wa Bunge la Katiba na Watanzania wengi kutaka kugeuza Katiba kama chombo/document ya kisera. Katiba ni sheria. Kwa mantiki hiyo, mambo ya sera yanaweza kujadiliwa nje ya Katiba.
Mfano, Bwana Makonda anadai "Nilidhani Rasimu itaweka bayana Uanzishwaji wa Baraza La Vijana la Taifa ili kiwe chombo cha kikatiba cha Vijana" . Ujinga huo. Kitu gani katika Katiba ya sasa inayowazuia vijana kujadili mambo yao au kuunda baraza lao la vijana? Kwa sababu hatujui maana ya Katiba, ndiyo maana akina Nape wanapiga kelele sera za CCM ziingizwe kwenye Katiba. Huo ni upunguani.