Katiba Si Sera

Mautino

Member
Joined
Feb 20, 2014
Posts
42
Reaction score
22
Sijui wewe, lakini mimi nakerwa sana na hili wajumbe wa Bunge la Katiba na Watanzania wengi kutaka kugeuza Katiba kama chombo/document ya kisera. Katiba ni sheria. Kwa mantiki hiyo, mambo ya sera yanaweza kujadiliwa nje ya Katiba.

Mfano, Bwana Makonda anadai "Nilidhani Rasimu itaweka bayana Uanzishwaji wa Baraza La Vijana la Taifa ili kiwe chombo cha kikatiba cha Vijana" . Ujinga huo. Kitu gani katika Katiba ya sasa inayowazuia vijana kujadili mambo yao au kuunda baraza lao la vijana? Kwa sababu hatujui maana ya Katiba, ndiyo maana akina Nape wanapiga kelele sera za CCM ziingizwe kwenye Katiba. Huo ni upunguani.
 


Hoja zako ni nzito Mautino wachangiaji wachache wanaziweza ndo maana wengi wameingia mitini wakachangie sera za CCM
 
Ni kweli Kiongozi! Hata mimi nashindwa kuelewa wanaposema " Hiki kipengele ndani ya Rasimu hakipo kwenye Sera yetu au Sera yetu ni Serikali mbili!" Sasa kama kila chama kitapigania kiingiza sera zake kwenye Katiba, hiyo itakuwa ni Katiba au Sera ya Vyama!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…