Katiba tunayo itaka

Katiba tunayo itaka

keulankubha

Member
Joined
May 7, 2012
Posts
49
Reaction score
13
MAONI YA KATIBA MPYA

Kwavile serikali imetambua/inatambua kuwa suala la katiba ni jambo muhimu sana, pia kuwa katiba ina husu wananchi hivyo na wananchi kutoa maoni yao ya katiba wanayo itaka na mfumo mzima wa uongozi/viongozi/watawara wao katika katiba mpya kwa mstakabali wa taifa kwa ujumla.

1. Jambo la kwanza la kuangalia majukumu ya Rais kwa ujumla katika katiba hii iliyopo ni makubwa sana. Mfano wa kuteua wakuu wa mikoa, wilaya, wakurugenzi na mawaziri.
2. Sioni kuwepo kwa wakuu wa mikoa na wilaya. Kwa mtazamo wangu sehemu moja iondolewe haina maana yoyote katika nchi changa kama hii Tanzania. Mtu wa kuondolewa ni mkuu wa wilaya tubaki na wakurugenzi wa wilaya na wakuu wa mikoa katika katiba hii mpya.
i) Pia wakuu wa mikoa wachaguliwe na wananchi katika mikoa yao, ili uwepo ushindani wa kuinua uchumi wa maendeleo ya mikoa, wilaya na taifa kwaujumla. Ili swala liingizwe kwenye katiba mpya. Viongozi hawa wakichaguliwa na wananchi watasimamia na kuimalisha uchumi na maendeleo ya mikoa, wilaya na kitaifa tena kwa ushindani mkubwa kwa masilai ya wananchi.

ii) Wakuu wa mikoa wasiwe wagombea wa chama chochote cha siasa katika katiba mpya.

RAIS TUNAYE MTAKA KATIKA KATIBA MPYA.
i) Rais awetayari kuwajibika na kufikishwa mahakamani itakapo bidi. Pia ikumbukwe kuwa katiba yetu haina chama, kiwe chama tawala au chama chochote cha siasa. Pia katiba yetu haina dini iwe dini ya kikristo au dini ya Islamic au taasisi yeyote ile.
ii) Katiba ioneshe wazi kuwa mtu yeyote anayeteuliwa kuwa mgombea urais awe amekubaliana na masharti ya katiba hii. Kuwa yuko tayari kuwajibika/kuwajibishwa na kufikishwa mahakamani pale itakapo bidi. Huyo ndiye rais tunayemtaka, sio kwamba tumsikilize yeye anayoyataka. Katiba hii mpya iweke wazi.

iii) Pia katiba mpya ioneshe wazi kuwa rais anao wajibu wa kuteua mawaziri kwa kuzingatia yafuatayo:-
a) Kwanza mawaziri/waziri atakaye teuliwa na rais awe chini ya uangalizi kati ya miezi sita (6) au muda usio zidi mwaka mmoja (1).
b) Baada ya miezi sita (6) au mwaka mmoja itakavyokuwa imepitishwa kabla ya kuapishwa kuwa waziri kamili, yawepo maoni ya wananchi kumkubali au kumkataa kulingana na utendaji wake wa kazi wa miezi sita (6) au mwaka mmoja aliokuwa katika uangalizi.

SPIKA WA BUNGE
Katiba mpya ipunguze mamlaka makubwa aliyonayo speaker wa bunge, kwa masilai ya wananchi na taifa kwa ujumla. mfano katiba iliyopo imempa mamlaka makubwa kuamua yeye atakavyo kulingana na mamlaka aliyonayo. Speaker wa bunge apewe mamlaka lakini yawe na mpaka. Pia maamuzi ya bunge yawe ndio ya mwisho maana bunge ni chombo kikuu kwa niaba ya wananchi kusimamia na kuishauri serikali katika utekelezaji wa majukumu yake kwa mjibu wa katiba.

SUALA LA MUUNGANO

Muungano ni jambo la msingi sana. Pia katiba hii mpya ioneshe/iweke wazi suala la muungano pasipokuwa na upendeleo wa aina yeyote ile maana katiba hii iliyopo sasa imetunyima haki kama sisi watanzania bara. Mfano Tanzania visiwani wana rais wao lakini Tanzania bara hatuna rais. Pili Zanzibar wana piga kura mara mbili kwa kumchagua rais wao pia kumchagua rais wa jamuhuri ya muungano.

Kuna mambo ya kufuata katika muungano kama ifuatavyo:-

a) Tuwe na rais mmoja wa jamuhuri ya muungano wa Tanzania.
b) Tuwe na serikali moja ya jamuhuri ya muungano wa Tanzania.

Kama hautakuwepo umuhimu wa kuwa na serikali moja ya jamuhuri ya muungano Tanzania basi tuwe na serikali tatu kama ifuatavyo:-
i) Tuwe na serikali ya Tanganyika
ii) Iwepo serikali ya Zanzibar
iii) Iwepo serikali ya jamuhuri ya muungano waTanzania

Katiba mpya itoe haki katika sehemu zote bila kujali cheo alichonacho mtu, mfano taratibu za kisheria zinazo tumika kwa mwananchi au walala hoi hiyo hiyo ndio itumike kwa watu wote, awe mfupi, mrefu, mwembamba, mnene au kiongozi/mtawara yeyote yule katiba ioneshe wazi kuwa njia za kisheria zinazotumika ndio zile zile zinazotumika kwa mtu yoyote yule bila kujali chama, kiwe chama tawara au chama chochote cha siasa, jinsia, kabira, wala dini yoyote ile.
 
Serekali mbili tuu, Tanganyika na Zanzibar end of the complexity!
 
Briliant observation comrade friend! Nakushauri uwasilishe maoni haya kwenye Tume. google tume ya mabadiliko ya katiba hapo utapata email address yao then drop maoni yako hapo! haya ndo maoni wanajamvi tunatarajiwa tuyatoe tuachane na siasa lets be objective!
 
Back
Top Bottom