Katiba, Wanatunyonga kwa Kamba yetu Wenyewe!

Katiba, Wanatunyonga kwa Kamba yetu Wenyewe!

Kijakazi

JF-Expert Member
Joined
Jun 26, 2007
Posts
7,093
Reaction score
10,469
Watu wote wanaofwatilia na kusubiri Katiba mpya wanapoteza muda wao wa thamani Buree!
Kwa sababu Siku zote anayeandika Katiba ndio anaamua kipi kiwemo na kipi kisiwemo, kwa maana nyingine ni kwamba Katiba siku zote ni kwa maslahi ya yule anayeitengeneza,
na haijawahi kutokea ktk historia ya Dunia hii Katiba ikatengenezwa kwa maslahi ya ngedere hata siku moja, na ndio maana mnaona kila siku kuna mapya na wanagombania Posho kwa maana wanajua hamna jipya hata Serikali inalijua hilo na tayari imeshahahakisha kwamba maslahi yake yanalindwa kwa vyovyote vile kwenye hiyo Katiba mpya, hiyo yote ya kuleta kwa Wananchi ni ktk kutaka kuwahadaa tu ile mwisho wa siku mkilalamika wawaambie tunafwata Katiba mliyoichagua nyinyi wenyewe, kwa maana nyingine wanawanyonga kwa Kamba yenu!
Mkitaka Katiba ya Kweli ni Msituni tu hakuna Njia nyingine!
 
Pale ziwa Victoria Mv Bkb ilizama lakini mpaka leo serikali haijawahi kuona umuhimu wa kuwasaidia watu wale waendelee kupata usafiri kwa kununua meli mpya ukiachilia mbali danadana zinazopigwa kila wa leo,zaidi nashangaa serikali hiyohiyo inapata laki 3 za kumlipa mjumbe mmoja kwa siku kwa siku 70 na kamwe serikali hiyohiyo haiko tayari kupunguza kiwango hicho walau wakasaidie kununua hiyo meli badala yake inasema asiye tayari kupokea hiyo pesa ajiondoe ..kwahiyo wakjiondoa ndo kutaleta meli mpya?
 
Back
Top Bottom