IsangulaKG
JF-Expert Member
- Oct 14, 2010
- 706
- 386
Mshangao mwingine niliouona katika rasimu hii ya katiba ni misingi ya kijamaa. Misingi inaonekana katika masharti ya viongozi kama wabunge kumiliki mali. Leongo na vipengele hivyo ni kuwafanya viongozi wawe wajamaa na kuleta usawa wa kimaisha kwa watu wote. Ukweli ni kwamba Mfumo wa Ujamaa HAUJAWAHI KULETA MAFANIKIO KATIKA NCHI YOYOTE. USSR ilianguka kutokana na ujamaa. China ujamaa ulishindikana na wameonyesha mafanikio kwa kuwa na mfumo mchanganyiko "mixed economy" na sasa wako kwenye masoko huria au "market capitalism"
Tanzania haiwezi kufanikiwa kwa misingi ya Kijamaa. Ni lazima tuwe na misingi inayochochea ushindani wa kiuzalishaji ili kukuza pato la taifa, na hatuwezi kuwa na misingi hiyo katika ujamaa. Katiba ilitakiwa ionyeshe kwa uwazi kuwa japo watanzania wanaishi kijamaa lakini uchumi unaendeshwa kwa mfumo wa market capitalism na lengo la serikali ni kuweka mifumo ya uzalishaji shindani ili tuweze kupenyeza bidhaa zetu katika masoko ya nje na kukuza GDP>
Najua ni wachache watakaonielewa!