Katiba ya ndoa/mahusiano

Katiba ya ndoa/mahusiano

Raia Fulani

JF-Expert Member
Joined
Mar 12, 2009
Posts
11,478
Reaction score
3,659
Majuzi kuna mkenya mmoja alitengeneza katiba yake kuainisha ni jinsi gani mpangilio wa maamuzi na uwajibikaji vinavyopaswa kuwa ndani ya nyumba. Aliandaa hiyo katiba baada ya kusumbuliwa na wanawake wa awali. Alizungumzia machache kwa ufasaha tu. Swali ni je, kuna haja ya kuwa na maandiko yanayotoa mwongozo wa majukumu ya baba, mama na watoto? Yawezekana ikaleta maridhiano baada ya kila mmoja (wazazi) kusoma, kuridhia na kusaini
 
Iko siku mtaanza kufikiria hata kusainishana kufanya tendo la ndoa
 
Kwa hiyo mmojawapo akikosea mahali,ataambiwa rejea kifungu flani! hata kuwe nakatiba itakayoshuka kutoka juu sidhani kama itasaidia.Vitabu vya dini pia ni katiba lkn imekuwa ngumu pia.

Kingi ningefurahi kuipata hiyo katiba niitoe complimentary kwa ndugu zangu wa ISC wawe na katiba mbili,sipati picha watakavyokuwa wanarejea huku na huku,,,lol
 
No! ndoa ni mkataba na mkataba lazima uwe na pande mbili ambazo ni baba na mama,mi naunga mkono lazima kuwepo na masharti ndani ya ndoa,hizi ndoa za misukumo ya ngono tuachane nazo, watu wanaoana hawamalizi mwezi kisa walisukumwa na kudanganyana na i love u i love u,watoto wapo mitaani kisa baba na mama waliachana,tubadilike vigezo na masharti lazima vizingatiwe,
 
It depends na watu wenyewe kama wameshindwa kufuata maandiko yaliyoko kwenye Biblia na Quran, Je? Unafikiri ukiweka hivyo vigezo na masharti vitafuatwa? Kama ni msukumo wa mtu kufanya kitu fulani yeye atafanya tu as long as anajisikia kufanya hivyo bila kuhisi mwenzake wa upande wa pili anajisikiaje, kama mnahitaji kuweka sheria basi ni vizuri kurejea kwenye Biblia na Quran maana zina sheria tosha ambazo kila mtu akifuata basi kutakuwa hakuna haja ya kuanza kufikiria katiba katika ndoa yako au mahusiano yako
 
Hivi ada yako ya mwezi huu umelipa maana mwezi ndio unaisha hivyo unajua kwenye chama chetu wewe ni mwanachama mtiifu sana kwahiyo tusingependa ukawa na malimbikizi ya madeni ya ngoja niwasiliane na katibu
 
nitaifanyia kazi kuibandika hapa. Ama kama kuna mdau anayo aiweke hapa idadavuliwe.
 
No! ndoa ni mkataba na mkataba lazima uwe na pande mbili ambazo ni baba na mama,mi naunga mkono lazima kuwepo na masharti ndani ya ndoa,hizi ndoa za misukumo ya ngono tuachane nazo, watu wanaoana hawamalizi mwezi kisa walisukumwa na kudanganyana na i love u i love u,watoto wapo mitaani kisa baba na mama waliachana,tubadilike vigezo na masharti lazima vizingatiwe,

Kabisa Man! na ikitokea vikavunjwa basi hadi mahakamani ifike na ikiwezekana adhabu kama faini au kifungo itolewe. Italeta heshima na kuwafanya watu wasiokuwa responsible wawe RESPONSIBLE.
 
Lol!!!!! I don't see this happening
 
It depends na watu wenyewe kama wameshindwa kufuata maandiko yaliyoko kwenye Biblia na Quran, Je? Unafikiri ukiweka hivyo vigezo na masharti vitafuatwa? Kama ni msukumo wa mtu kufanya kitu fulani yeye atafanya tu as long as anajisikia kufanya hivyo bila kuhisi mwenzake wa upande wa pili anajisikiaje, kama mnahitaji kuweka sheria basi ni vizuri kurejea kwenye Biblia na Quran maana zina sheria tosha ambazo kila mtu akifuata basi kutakuwa hakuna haja ya kuanza kufikiria katiba katika ndoa yako au mahusiano yako
Kaka kakudanganya nani watoto wa sikuhizi wanaogopa hivyo vitabu vitakatifu? unajua binadamu tumeumbwa na aibu na kweli kama mtu alikubali kwa dhati kabisa kwamba nakubaliana na masharti haya sidhani kama atayakiuka,na akikiuka anajua lazima atasutwa
 
Nakuona unavyokuja vizuri,big up my gud boy!nitawatuma kina Kaizer,Acid,Roy, Asprin etc waje wajifunze kwako:smile-big:
 
Hivi ada yako ya mwezi huu umelipa maana mwezi ndio unaisha hivyo unajua kwenye chama chetu wewe ni mwanachama mtiifu sana kwahiyo tusingependa ukawa na malimbikizi ya madeni ya ngoja niwasiliane na katibu

Naona unachanganya na kule ulikotoka,hiki chama kipya ulichoko hakina michango ya mwezi mpendwa.
Usisahau baadae ni zamu yako kuongoza kipindi,ikibidi waalike na wenzio.
 
Kaka kakudanganya nani watoto wa sikuhizi wanaogopa hivyo vitabu vitakatifu? unajua binadamu tumeumbwa na aibu na kweli kama mtu alikubali kwa dhati kabisa kwamba nakubaliana na masharti haya sidhani kama atayakiuka,na akikiuka anajua lazima atasutwa

kusutwa tu? Na adhabu pia
 
Naona ndoa zetu zimekosa maana halisi kabisa
dunia imebadilika hatufati hata maagizo ya mungu
tunatafuta fomula zetu binafsi
ndoa nyingi zinavunjika ,upendo umekoma,chuki zimejaa ndani ya wanandoa ,kwa sababu ya kiburi majivuno kujiona bora
tunakoelekea ndio huko kwenye ndoa za mikataba kwa sababu ya utandawazi ,kila mmoja kujiona zaidi mwenzio
eeh mungu tusaidie
 
Na hapo ndipo mnapokosea mnakimbilia kuweka sheria zenu wenyewe wakati zile zilizoko kwenye vitabu vya dini hamzifuati, tusianze na visingizio eti ohooo binadamu ameumbwa na aibu, anza kufuata kwanza sheria alizoziweka Mungu ndio mambo mengine yatafuata kama wewe ni mkristu fuata zile amri kumi kama muislamu pia wao wana sheria zao katika dini zao
 
Well said FL1 you deserve a round of applause
 
Na hapo ndipo mnapokosea mnakimbilia kuweka sheria zenu wenyewe wakati zile zilizoko kwenye vitabu vya dini hamzifuati, tusianze na visingizio eti ohooo binadamu ameumbwa na aibu, anza kufuata kwanza sheria alizoziweka Mungu ndio mambo mengine yatafuata kama wewe ni mkristu fuata zile amri kumi kama muislamu pia wao wana sheria zao katika dini zao

amri za Mungu ziko miaka mingapi ndugu? Hata kutunga hiyo katiba si kama inaenda kinyume na amri zake. Tofauti ni kuwa amri za Mungu ziko general na abstract zaidi wakati katiba ya wanandoa itakuwa specific na more visible
 
Naona ndoa zetu zimekosa maana halisi kabisa
dunia imebadilika hatufati hata maagizo ya mungu
tunatafuta fomula zetu binafsi
ndoa nyingi zinavunjika ,upendo umekoma,chuki zimejaa ndani ya wanandoa ,kwa sababu ya kiburi majivuno kujiona bora
tunakoelekea ndio huko kwenye ndoa za mikataba kwa sababu ya utandawazi ,kila mmoja kujiona zaidi mwenzio
eeh mungu tusaidie

dada hujatoa suluhu. Umesononeka tu. Kama wanandoa wanashindwa kufuata matakwa ya Mungu wafanye nini?
 
amri za Mungu ziko miaka mingapi ndugu? Hata kutunga hiyo katiba si kama inaenda kinyume na amri zake. Tofauti ni kuwa amri za Mungu ziko general na abstract zaidi wakati katiba ya wanandoa itakuwa specific na more visible

Zipo muda mrefu lakini hilo sio swala la kujiuliza swala la kujiuliza ni je zinafuatwa? Na kama hazifuatwi unafikiri hiyo katiba ya wanandoa ndio itafuatwa kwa vile itakuwa specific na more visible, just follow what GOD needs you to do and the rest will fall upon you, kama mnamshirikisha Mungu katika masuala yenu na kila mtu anajua wajibu wake sidhani kama kuna haja ya suala la katiba, na mtu kushindwa kufuata matakwa ya Mungu si kigezo cha kuanzisha katiba kama ameshindwa kufuata maagizo ya Mungu hiyo katiba ambayo utakayotunga ndio unahisi kuwa ataweza kuifuata suala hapa ni kuwa kama ni hulka ya mtu atafanya tu no matter what you do
 
Back
Top Bottom