Katiba ya Tanganyika inawezekana kwa miezi mitatu

Katiba ya Tanganyika inawezekana kwa miezi mitatu

MWALLA

JF-Expert Member
Joined
Dec 12, 2006
Posts
16,952
Reaction score
10,500
Dar es Salaam. Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Jaji Joseph Warioba amesema Katiba ya Tanganyika inaweza kuandikwa ndani ya miezi mitatu tu kwa kuwa maoni mengi yaliyomo katika Rasimu ya Katiba iliyozinduliwa Jumatatu, kwa kiwango kikubwa yametoka kwa wananchi wa upande huo wa Muungano.

Warioba alisema hayo jana wakati akizungumza na Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF), kwenye Ukumbi wa Karimjee, jijini Dar es Salaam.

"Kutunga Katiba ya Tanganyika siyo kazi ngumu, ukisoma rasimu hii sura ya kwanza mpaka ya tano, sioni kama Katiba ya Tanganyika itakuwa tofauti na maoni yaliyomo katika sura hizo," alisema na kuongeza:

"Misingi iliyopo katika utangulizi wa rasimu hii imetokana na maoni ya wananchi hao. Wakati wa kukusanya maoni, Zanzibar walijikita zaidi kwenye Muungano, maoni mengine kwa kiwango kikubwa yametoka kwa Watanzania Bara na katika kuandika Katiba ya Tanganyika sioni kama watabadilisha chochote kuhusu misingi hii ambayo ni; tunu za taifa, maadili, malengo na haki za binadamu."

Alisema kuhusu kubadilishwa kwa mihimili ya Serikali na vyombo vingine vya kitaifa, kikubwa kinachoweza kuguswa ni muundo wa Bunge la Tanganyika, Baraza la Wawakilishi Zanzibar na Baraza la Mawaziri.

"Kuhusu taratibu za kufanya kazi; iwe ni madaraka ya Rais, utaratibu wa kufanya kazi katika Bunge, Mahakama na Serikali sioni kama litakuja suala jipya kwa sababu mambo hayo yameshatolewa maoni. "Kilichobaki ni madaraka kwa umma tu, kwa maana ya Local Government (Serikali za Mitaa). Hata hili la madaraka kwa umma watakaolishughulikia watumie taarifa za wananchi waliotoa maoni yao kuhusu Katiba Mpya. Wananchi walitoa maoni kuhusu jambo hili ambayo yapo wazi kabisa."

Uchaguzi Mkuu 2015

Kuhusu uwezekano wa Katiba Mpya kutumika katika Uchaguzi Mkuu 2015, Jaji Warioba alisema Tume hiyo ilipewa muda mfupi wa kuandaa Rasimu ya Katiba kwa sababu ilielezwa kuwa uchaguzi wa mwaka 2015, utafanyika kwa kutumia Katiba Mpya.

"Katiba hii ilitakiwa iwe imekamilika Aprili mwaka huu, maana yake tungekuwa na mwaka mmoja na nusu wa kufanya mambo mengine ya kuwezesha itumike kwenye uchaguzi wa mwaka 2015," alisema.

Alisema ndiyo maana katika rasimu hiyo, Tume imeweka masharti ya mpito ya miaka minne, kuanzia siku inapopatikana Katiba Mpya hadi Desemba 28, 2018.

Alisema rasimu hiyo imefafanua Baraza la Mawaziri na Bunge vitakuwaje… "Sasa hivi tuna Serikali na Bunge. Katiba Mpya itapatikana mwaka huu, lakini Bunge letu litaendelea kuwapo kwa msingi wa Katiba ya sasa mpaka ufike wakati wa uchaguzi, hiyo inafanyika kwa ajili ya kulinda uongozi wa Bunge na Serikali."

Alisema ili kuwepo na Uchaguzi Mkuu kwa Katiba Mpya ni lazima itungwe Katiba ya Tanganyika, kwamba wamependekeza miaka minne ya mpito ili kutoa nafasi ya kubadilishwa kwa mambo kadhaa, ikiwa ni pamoja na kuundwa upya Tume ya Uchaguzi itakayoendesha uchaguzi kwa msingi wa Katiba Mpya

 
Kiini macho.
Ni kiini macho. Process ni ile ile kwanza kutunga sheria ya kuunda katiba mpya,kuunda tume, kukusanya maoni, kutoa rasimu ya kwanza, mabaraza ya katiba, rasimu ya pili, bunge la katiba.

Short kati itakua kutumia tume ya sasa ukiondoa wajumbe wa Zanzibar ili watoe rasimu ya kwanza halafu ndo maoni yatolewe. Hapa hakutakuwa na ukusanyaji wa maoni ya awali, assuming that mengi yalishatolewa.

Kwa ufupi si chini ya mwaka kama mambo yataenda fasta.
 
Nashauri katiba ya Tanganyika inatakiwa kukusanywa maoni ya wananchi siyo watu wakajifungie ofisini kama ile ya mwaka 1977 hafu watuletee et ndo katiba yenu. Hatutaki tena kutudictate
 
Huyu mzee naona amenogewa posho sasa anataka aunganishe na shughuli ya kuandika katiba ya Tanganyika. Yale maoni yalitolewa katika muktadha wa Muungano na siyo lazma watananyika tukubaiane nao yotekammzee anavyotaka kutuainisa. Pili huu mchakato ulishirikisha na wajumbe wazanzibari kuandaa rasimu ya sasa. Watanganyika tuna wajibu na haki ya kujadili mustakabi wao bila kuingiliwa wala kuwashirikisha wazanzibari kama ilivyokuwa kwa kamati ya Warioba.
 
Mimi nakubaliana na Judge Warioba kwamba maoni mengi yameshatolewa kwenye hii Katiba ya Muungano.

Lakini angekwenda hatua moja zaidi, kwakuwa inasemekana kwamba katiba nzuri kabisa kwa nchi za Afrika ni Katiba za Kenya na Ghana. Basi tutumie maoni ya tume ya Judge Warioba plus katiba za Kenya na Ghana kwa maana ya kuzihuhisha katika mazingira ya Tanganyika kutengeneza katiba mpya ya Tanganyika.

Tukishapata RASIMU ya katiba mpya ya Tanganyika ambayo imetokana na maoni ya tume ya Warioba plus katiba za Kenya na Ghana basi ipelekwe kwenye bunge la katiba ambalo litakuwa na wabunge kutoka Tanganyika tu kabla ya kuletwa kwa watangayika kupigiwa kura ya NDIYO NA HAPANA.

But the bottom line ni kwamba kwa mda huu uliobaki < 2 years sioni tukiipata katiba mpya ya Tanganyika kabla ya general election October 2015.
 
Warioba alichotumwa kwa mujibu wa Sheria ni kukusanya maoni kuhusu uundwaji wa Katiba ya JMT! Hayo ya kukusanya maoni kuhusu Katiba ya Tanganyika ameyafanya kwa mujibu wa Sheria ipi?
 
Wazanzibr ni walimu wenu watanganyika kwenye siasa,mlilala sana,koti la muungano mlilokuwa mmejifichia tayari tumelimwagia petrol muda wowote tunalipiga kibiriti,zanzibar c tanganyika.
 
Back
Top Bottom