abdulahsaf
JF-Expert Member
- Aug 31, 2010
- 858
- 130
Written by administrator // 31/03/2011
Na Dkt. Harith Ghassany
Leo nawaletea baadhi ya nakala za barua asilia kutoka nyaraka za Umoja wa Mataifa (UN), zenye kuthibitisha mtiririko wa kuwepo kwa uwanachama wa Tanganyika uliofuatiliwa na Uhuru wa Tanganyika uliopatikana tarehe 9 Disemba 1961; Uhuru wa Zanzibar uliopatikana tarehe 10 Disemba 1963; Jamhuri ya Muungano wa Tanganyika na Jamhuri ya Watu wa Zanzibar, ilioundwa tarehe 26 Aprili 1964; na kuanzishwa kwa jina la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, tarehe 2 Novemba 1964.
Napenda kuwatahadharisha wote watakayoyasoma makabrasha haya watahadhari na kutumbukia ndani ya mjadala wa lawama, makosa yaliofanyika huko nyuma, na wahusika wa makosa hayo. Wao watahukumiwa kwa yao, na sisi tutahukumiwa kwa nia, uwezo, na maamuzi ya pamoja ya Wazanzibari ulimwenguni kote, kuwataka viongozi na wananchi wa Zanzibar kutoa msimamo wa pamoja na kuamua kuirudishia Zanzibar haki zake za Kitaifa na za Kimataifa.
Maelezo ya nyaraka:
Siku hiyo birthday boy hatohudhuria kunako sherehe za aina yake na badala yake atahudhuria mtu ambaye anaitwa Tanzania aliyezaliwa tarehe nyingine na kwa jina jingine.
Huu (hivi sasa) ndio wakati wa kufanya maamuzi maamuzi makubwa ya kuirudishia Zanzibar haki zake za Kitaifa na za kimataifa kupitia Katiba ya Zanzibar. Tunaweza kuamua kuchagua jambo moja kati ya haya matatu:
a) Tuitekeleze rasimu ya Katiba Mpya itakayozifanya Zanzibar na Tanganyika (haipo) kuwa ni Mikoa itakayotawaliwa na Magavana?
b) Tulisubiri gari la Katiba ya Muungano litakaloanza kusukumwa 2014 na kupigwa moto (start) na mrithi wa Rais Kikwete baada ya uchaguzi wa 2015?
c) Au tuamue kuipa nguvu Katiba ya Zanzibar na kuipigia Kura ya Maoni hivi sasa ambayo ndio Dira ya Zanzibar itakayoirudishia Zanzibar madaraka yake ya Kitaifa na ya Kimataifa? Na baadae ndio Zanzibar ikae na Jamhuri ya Tanganyika iliojifichua na yenye Katiba yake, kuujadili Mkataba (Treaty) wa Mashirikiano kama ule wa Umoja wa Ulaya (European Union)?
Nakutakieni usomaji mwema wa nyaraka za Umoja wa Mataifa.
Nyaraka:http
://www.mzalendo.net/makala/katiba-ya-zanzibar-ndio-dira-ya-zanzibar
#gallery-1 { MARGIN: auto}#gallery-1 .gallery-item { TEXT-ALIGN: center; MARGIN-TOP: 10px; WIDTH: 33%; FLOAT: left}#gallery-1 IMG { BORDER-BOTTOM: #cfcfcf 2px solid; BORDER-LEFT: #cfcfcf 2px solid; BORDER-TOP: #cfcfcf 2px solid; BORDER-RIGHT: #cfcfcf 2px solid}#gallery-1 .gallery-caption { MARGIN-LEFT: 0px}

- Barua kutoka kwa Waziri Mkuu wa Tanganyika, Julius Nyerere kuomba uwanachama Umoja wa Mataifa baada ya Tanganyika kupata Uhuru wake kutoka kwa Muingereza tarehe 9 Disemba, 1961.
- Azimio la Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa ya kuikubalia Tanganyika kujiunga na Umoja wa Mataifa.
- Barua kutoka kwa Waziri Mkuu wa Zanzibar, Sheikh Muhammed Shamte kuiombea Zanzibar uwanachama Umoja wa Mataifa baada ya Zanzibar kuupata Uhuru wake kutoka kwa Muingereza tarehe 10 Disemba, 1963.
- Azimio la Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa ya kuikubalia Zanzibar kujiunga na Umoja wa Mataifa kuanzia tarehe 16 Disemba, 1963.
- Barua kutoka Wizara ya Nchi za Nje ya Jamhuri ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar yenye kuiarifu Umoja wa Mataifa kuwa nchi mbili, Jamhuri ya Tanganyika na Jamhuri ya Watu wa Zanzibari, zimeungana na kuwa nchi moja chini ya Uraisi wa Mwalimu Julius K. Nyerere. Barua inatoa taarifa kuwa Khati za Muungano zilithibitishwa na Bunge la Tanganyika na Baraza la Mapinduzi la Jamhuri ya Watu wa Zanzibar.
- Barua yenye kuomba usajili wa Khati za Muungano baina ya Muungano wa Jamhuri ya Tanganyika na Jamhuri ya Watu wa Zanzibar kwa mujibu wa kifungu 102 cha United Nations Charter.
- Barua yenye muhuri wa Jamhuri ya Tanganyika wenye tarehe 2 Novemba 1964, yenye kuiarifu Umoja wa Mataifa kuwa jina la Jamhuri ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar limegeuzwa na kuitwa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
- Muhuri wa Jamhuri ya Tanganyika uliopigwa New York, tarehe 2 Novemba, 1964.
- Taarifa ya habari ya Umoja wa Mataifa kuhusiana na kubadilishwa kwa jina kutoka Jamhuri ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar kuelekea Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.