Katiba yetu inavyotisha Wabunge

Katiba yetu inavyotisha Wabunge

Shujaa Mwendazake

JF-Expert Member
Joined
Jul 11, 2015
Posts
4,016
Reaction score
6,759
Spika Job Ndugai amesema kwa mujibu wa Ibara ya 90(2)(b) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Rais ana uwezo wa kuvunja Bunge endapo likikataa kupitisha Bajeti ya Serikali.

Nimejiuliza maswali
1. Kuna ulazima wowote wa Spika Ndugai kutoa leads Kwa wabunge cha kufanya? Spika wa Bunge anapaswa kuwa neutral ili Demokrasia ionekane Bungeni. Sasa Bajeti hii ikipita Kwa kauli hii huku nje tafsiri itakuwa wabunge wameogopa kuvuliwa Ubunge.

2. Katiba yetu inakinzana Moja kwa Moja na dhana ya Demokrasia ndani ya Bunge. Bado katiba yetu haijafungua Milango ya Demokrasia maeneo Mengi nchini.

3. Kuna haja ya Wabunge Kila mmoja kulipwa Milioni 34 plus kwenye Kikao hiki cha Bunge la budget tu halafu ikifika kupiga kura anaambiwa usipopiga ya ndio na Bajeti isipopita utavuliwa Ubunge? Hebu chukua hiyo hela Zidisha mara Wabunge 300 tu.

4. Wabunge wametoa mapendekezo kwenye budget hii na huku nje wananchi wametoa Mapendekezo nini kifanyike lakini kwa ibara hii ya katiba mapendekezo yote Waziri anaweza kuyatupilia mbali as Long as Katiba itawachinja wabunge wote kama wataikataa Bajeti. Hapa ndipo Katiba inapompa kiburi Waziri.

Ole Mushi
0712702602.
 
Back
Top Bottom