Katiba yetu ndiyo inayowafanya wastaafu kulalamika

Katiba yetu ndiyo inayowafanya wastaafu kulalamika

Elius W Ndabila

JF-Expert Member
Joined
Jul 17, 2019
Posts
324
Reaction score
649
KUNA UHUSIANO WA CHEO NA UWEZO WA KUAMUA?

Na Elius Ndabila
0768239284

Ni kawaida kwa sasa na umekuwa ni utamaduni Kwa Mtu akifukuzwa kazi, Akistaafu, Akistafishwa au Kwa sababu zingine zozote mtu asipo kuwa kwenye nafasi anakuwa mshauri mzuri wa mambo ya nchi kuliko alipokuwa kiongozi.

Kumekuwa na mijadala mikubwa ya pande mbili kuzungumzia uhalali wa ushauri unaokuja baada ya kutokuwa kwenye nafasi. Kwenye two School of thought wapo wanaoungana na hoja juu ya dhima ya wanachoshauri na Wapo wanaopingana na wanachoshauri kuwa nia(intent) yao ingekuwa njema basi wangeshauri wanapokuwa kwenye uongozi ambapo wanakuwa audible kuliko ukiwa nje unapokuwa voiceless.

Je, kunakuwa na nia njema au ovu? Actus reus and mens Rea? Hili si mtazamo wangu Kwa leo

Leo sahau kuhusu UKIROBOTO NA UHUNI, ninazungunza jambo kubwa ambalo inaweza kuwa majibu ya two school of thought.

Sisi Wamalila tunamsemo wetu tunasema, UTALONGAJE INGA USUNTILE ISHAKULYA MWILOMU, kwa tafsiri isiyo rasimi ni kuwa USIZUNGUMZE KAMA UMEWEKA CHAKULA MDOMONI.

Tafsiri yake ni kuwa unapokuwa kwenye uongozi huwezi kujua sana kilio Cha watu ambao wapo nje ya uuongozi

Unapotembelea V8 kama ya Kaka Yangu Polepole enzi hizo basi ni ngumu kujua shida ya mtembea Kwa miguu. Wenye V8 wakichukua ndipo akili inaanza kukukaa sawa na kuungana na wale ambao mwanzo uliwaona hawana maana.

Ninaamini, uwezo wa kuona na kuchambua mambo ungekuwa ni mkubwa tukiwa viongozi basi changamoto nyingi za nchi zingekuwa zimepata majibu. Mfumo wa Sheria zetu hasa katiba tuliyonayo inamfanya kila mtu kujipendekeza Kwa aliye juu yake ili asije akamtapisha tonge.

VEO atajipendekeza Kwa WEO, WEO atajipendekeza Kwa DED, DED atajipendekeza Kwa DC au RAS hivyo hivyo na wengine. Pengine tiba ya watu ili kuweza kufanya kazi bila unafiki, basi tiba ni KATIBA itakayotoa nafasi ya watu kuyaona yale ambayo yanaonwa wakistaafu. Wiki mbili zilizopita nilimuona Mbunge mmoja akikosoa, Juzi hapa nimemuona Polepole, Wiki iliyopita nimemuona Mstaafu mwingine akisema Wahitimu wa Vyuo vikuu wasiojiajiri ni Wahujumu, pia kwenye Kitabu Cha Hayati Ben ametoa mapendekezo ambayo alitamani yafanyiwe kazi.....na mifano mingine kadhaa.

Ukitazama Kwa jicho la tatu utagundua wengi wanapokuwa kwenye nafasi wanakuwa Wazalendo wa Vyeo na si Wazalendo wa Taifa. Wangekuwa Wazalendo Kwa Taifa basi wanayoshauri baada ya kustaafu walupaswa kuyashauri wakiwa kwenye nafasi na si baada ya kustaafu.
 
Back
Top Bottom