Katiba yetu ni shamba nono linalonufaisha kizazi cha watu fulani, marafiki zao na washkaji zao

Katiba yetu ni shamba nono linalonufaisha kizazi cha watu fulani, marafiki zao na washkaji zao

Mwande na Mndewa

JF-Expert Member
Joined
Feb 26, 2021
Posts
1,117
Reaction score
3,153
Hii katiba iliyopo ni shamba, ni mradi kuna watu wanaifurahia wao na vizazi vyao, wao na rafiki zao, wao na washikaji zao, kwa hiyo wasingependa kuiona ikibadilika kwa sababu ndiyo shamba lao watakula wapi? Na hili shamba ni kubwa na nono, ndiyo maana kila siku tunapigwa danadana. Lakini jambo lingine hii Katiba imekuwa lidude linatisha viongozi, kila kiongozi anayejaribu kuuendea huu mchakato anaanza halafu baada ya hapo anaipiga chini."

Hilo ni kweli kabisa. Kila mtu au nchi kwenye Muungano atatetea kifungi/vifungu vya Katiba kinomridhisha.
Kule Marekani ni nchi ya Muungano kama sisi. Katika Muungano wao wa nchi/states 50 kuna State kubwa ya California yenye Senators 2 na Wabunge 52 na State ndogo ya Wyoming yenye Senators 2 na Mbunge 1 tu.

Wakipiga Kura Wabunge 52 wa California kupitisha Sheria watapingwa na Mbunge 1 tu kutoka Wyoming. Lakini kwenye Senate Senators 2 wa California wakipendekeza Sheria inaweza kupingwa na Senators 2 kutoka Wyoming na kusababisha kutokupita.

Watu 49 Millioni wa California wanataka kipengele hicho cha Katiba kibadilishwe lakini Wyoming na States ndogo zaidi ya 26 wenye Senators 52 kati yao Wanapinga.

Utata huo utaendelea kuwepo kwa sababu States ndogo zinalinda Maslahi yao.
 
Back
Top Bottom