Kisheria na kwa mujibu wa "Articles of the Union" hakuna Katiba ya Tanzania, Kuna Katiba ya mpito ilioazimwa kutoka Katiba ya Tanganyika. Katibahiyo ya mpito imeishi kwa mabavu kwa miaka 53 sasa kinyume na makubaliano ya Muungano.
Hilo kwanza ulitambue kabla hujajikita kwenye " editorials errors"
Sio kweli, katiba ya mpito ni ile katiba iliyotumika toka baada ya muungano hadi mwaka 1977.
Mwaka huo wa 1977, ndipo katiba hii iliyopo sasa ilipitishwa, hivyo katiba ya mpito ilidumu kwa miaka 13 tuu toka ile 1964 hadi 1977.
Katiba iliyopo sasa imedumu kwa miaka 43 na sio 53!.
Na kwa upande wa Zanzibar, tangu baada ya yale Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar yaliyo mng'oa Sultan na utawala dhalimu wa mvamizi Mwarabu kwenye visiwa vile alipotoka kwao Oman na kuivamua kwa kuitwaa Zanzibar kama ameiokota ule mwaka 1832, mwaka 1964 ndipo wenyewe wenye Zanzibar yao, wakaikomboa toka makucha ya mvamizi, kupitia yale Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar ya January 12, mwaka 1964, Zanzibar ilitawaliwa kwa katiba ya mpito kwa miaka 20, hadi 1984 ndipo wakapitisha hii katiba ya Zanzibar inayotumika hadi sasa.
Ila Wanzanzibari ni watu wa ajabu sana kwasababu tangu baada ya muungano Zanzibar ilikuwa sio nchi bali ni sehemu ya JMT, lakini mwaka 2010, walifanya marekebisho ya katiba ya Zanzibar kwa kuchomekea vifungu kibao vinavyokwenda kinyume na katiba ya JMT, ikiwemo kujiita Zanzibar ni nchi na kutangaza mipaka yake, na kumuita Rais wa Zanzibar ni rais wa nchi ya Zanzibar na Amiri jeshi Mkuu wa Majeshi ya Zanzibar ya JKU, KMKM na Vikosi za SMZ!.
Kwa vile marekebisho hayo, yamekiuka katiba ya JMT, mpaka leo, mpaka kesho, katiba ya JMT haiyatambui marekebisho hayo, kwasababu ukweli unabaki kuwa ukweli kuwa Zanzibar sio nchi bali ni sehemu ya JMT, yenye utawala wake wa ndani ambao JMT haipaswi kuingilia!. Kujiita nchi wakati sio nchi, hakuna tatizo, hata migambo ya JKU na KMKM kuitwa jeshi, pia hakuna tatizo, Tanzania ni nchi moja tuu ya JMT, chini ya rais mmoja wa JMT na Amiri Jeshi Mkuu wa majeshi ya ulinzi na usalama.
P