Baraza la Wanawake wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo BAWACHA limewataka wanawake kujitokeza kwa wingi kushiriki maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani yatakayofanyika Machi 8, 2025, katika Ukumbi wa Mlimani City, Dar es Salaam.
Akizungumza na waandishi wa habari, Katibu Mkuu wa BAWACHA Taifa, Pamela Maassay, amesema maandalizi yanaendelea katika ngazi zote za chama, huku msisitizo ukiwa ni kushirikisha idadi kubwa ya wanawake kutoka kila kona ya nchi.
"Tumejipanga kuhakikisha tunakuwa na maadhimisho yenye tija na yenye ujumbe mzito wa kuhamasisha usawa wa kijinsia. Tunatarajia wanawake wasiopungua 3,000 kuhudhuria, na tunawaomba viongozi wa mikoa, majimbo na kata kuhamasisha ushiriki wa wanawake kwa wingi," alisema Masay.
Ameongeza kuwa mgeni rasmi wa tukio hilo atakuwa Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa, Tundu Lissu, akifuatana na viongozi wa chama pamoja na wageni waalikwa kutoka ndani na nje ya nchi.
Kaulimbiu ya mwaka huu ni "Kuharakisha usawa wa kijinsia kwa maendeleo endelevu," ambapo BAWACHA itatumia jukwaa hilo kuonesha mchango wa wanawake katika siasa, uchumi na jamii kwa ujumla.
Aidha, Maassay ameeleza kuwa moja ya ajenda kuu katika maadhimisho hayo ni kampeni ya "He for She," inayolenga kuwashirikisha wanaume katika kuhakikisha wanawake wanapata fursa sawa na kushiriki kikamilifu katika ujenzi wa Taifa.
"Kwa miaka mingi, harakati za haki za wanawake zimekuwa zikiendeshwa na wanawake wenyewe, lakini sasa tunasisitiza kuwa huu ni wakati wa wanaume pia kushiriki kwa nguvu zote katika kusukuma mbele ajenda ya usawa wa kijinsia," alisisitiza.