Pre GE2025 Katibu CCM, Iringa: Wenezi acheni kuwa Machawa na kubeba Mabegi ya Wagombea

Pre GE2025 Katibu CCM, Iringa: Wenezi acheni kuwa Machawa na kubeba Mabegi ya Wagombea

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)

Waufukweni

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2024
Posts
2,060
Reaction score
5,648
Katibu wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Iringa Vijijini, Sure Mwasanguti, amewataka wenezi wa chama hicho kuzingatia kanuni na miongozo ya CCM na kutokujihusisha na masuala ya kuwa machawa wa wagombea na kubeba mikoba yao kabla ya muda wa kikanuni.
IMG_2775.jpeg

Mwasanguti ameyasema hayo katika semina elekezi kwa makatibu wenezi wa matawi 89 na kata 15 katika Jimbo la Kalenga, iliyoandaliwa na Idara ya Wenezi Wilaya ya Iringa Vijijini, chini ya uongozi wa Mwenezi wa CCM Wilaya hiyo, Anord Mvamba.

Soma, Pia: Iringa: Matukio Yanayojiri Kuelekea Uchaguzi Mkuu wa 2025

Amesema kuwa, Jimbo la Kalenga lina Mbunge Mheshimiwa Jackson Kiswaga pamoja na madiwani, hivyo wenezi wanapaswa kushirikiana na viongozi walioko madarakani na kuepuka kujihusisha na shughuli za uchawa kwa wagombea.
IMG_2774.jpeg
Vilevile, amesisitiza kuwa hatua kali za kikanuni zitachukuliwa kwa wenezi watakaobainika kuanza kuunga mkono wagombea binafsi au kubeba mikoba ya wagombea katika mchakato wa uchaguzi.

"Chama cha Mapinduzi kina kanuni na utaratibu wake. Wenezi wanapaswa kuzingatia miongozo ya chama na kutoshiriki katika masuala ya uchaguzi kwa maslahi binafsi," alisisitiza Mwasanguti.
IMG_2776.jpeg
 
Back
Top Bottom