Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)
Katika hatua ya kuimarisha maendeleo ya wanawake mkoani Kilimanjaro, Mbunge wa Viti Maalum wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Ester Maleko, amekabidhi mashine 169 za kutotoleshea vifaranga vya kuku (incubator) kwa kila kata ya mkoa huo, ikiwa ni sehemu ya kutimiza ahadi yake ya kuinua wanawake kiuchumi kupitia ufugaji wa kuku.
Katibu wa Chama cha Mapinduzi (CCM) mkoa wa Kilimanjaro Merce Mollel akibariki msaada huo kwa kuwataka Wanawake katika mkoa huo kuchanganya siasa na shughuli za kiuchumi ili kuongeza ushiriki wao katika maamuzi ya Taifa.