Katibu Dorothy Semu (ACT Wazalendo): CCM/Serikali acheni kupotosha, uchumi haukui

Katibu Dorothy Semu (ACT Wazalendo): CCM/Serikali acheni kupotosha, uchumi haukui

Suphian Juma

Senior Member
Joined
Apr 2, 2019
Posts
140
Reaction score
577
Serikali Iache Upotoshaji Takwimu za Pato la Taifa

Ndugu Wanahabari,

Mtakumbuka Kamati Kuu ya ACT Wazalendo iliyokaa Oktoba 27, 2017 ilifanya uchambuzi juu ya hali ya uchumi wa nchi yetu, na taarifa juu ya Uchambuzi huo kutolewa kwa umma kupitia mkutano nanyi uliofanywa na Kiongozi wa Chama, ndugu Zitto Kabwe, Oktoba 28, 2017.

Uchambuzi wetu huo ulijikita katika kuonyesha kuwa uchumi wa nchi yetu ulikuwa unasinyaa na kusababisha ugumu wa maisha kwa wananchi, na kwamba uchambuzi wa taarifa zinazotolewa na NBS na BOT ulikuwa unaonyesha ukuaji wa Uchumi kwa robo ya Pili ya mwaka 2017 ni 5.7% tu na si 7.8% iliyotangazwa na Serikali.

Kufuatia uchambuzi wetu ule, Kiongozi wa Chama, ndugu Zitto alikamatwa na Jeshi la Polisi akituhumiwa kukiuka Sheria ya Mtandao (Cyber Crime Act) pamoja na Sheria ya Takwimu ya mwaka 2015 (Statistics Act), na mimi Katibu Mkuu wa ACT Wazalendo, Dorothy Semu, pamoja na Mwenyekiti wa Chama, ndugu Yeremiah Maganja tulihojiwa na kitengo cha makosa ya kifedha kwa makosa ya saa ya takwimu na sheria ya makosa ya mitandao kwa niaba ya wajumbe wa Kamati Kuu wa ACT Wazalendo (mimi kama Katibu wa Kikao na Mwenyekiti kama muongozaji wa Kikao husika).

Jeshi la Polisi pia lilichukua simu ya Kiongozi wa Chama, pamoja na Komputa ya Ofisi kwa madai ya kufanya uchunguzi, vitu hivyo havijarudishwa mpaka leo. Lakini pia Polisi walishindwa kutushaki Mahakamani kwa sababu sheria ya takwimu haikuwa kosa la kufanya uchambuzi wa taaarifa za BOT.

Disemba 13, 2017 Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF) liliitaka Serikali itazame upya vyanzo vyake vya takwimu za uchumi ili kupata picha halisi ya Hali ya uchumi wa Taifa letu. IMF pia walithibitisha kuwa ukuaji wa uchumi wa Tanzania unashuka, kutokana na viashiria vingine vya uchumi, na kwamba takwimu za Serikali ni lazima zitazamwe upya.

Mwezi Agosti, 2018 Serikali ilileta Bungeni mabadiliko ya sheria ya Takwimu kwa kufanyia marekebisho ya Takwimu ya mwaka 2015 na kuweka adhabu ya faini na kifungo kwa kufanya Uchambuzi tu wa taarifa za kitakwimu kama tulivyofanya ACT Wazalendo. Kifungu kipya cha 24A kililetwa kwa lengo la kuzuia uchambuzi huru wa takwimu zozote zilizotolewa. Mabadiliko hayo ya Sheria yaliweka udhibiti kuwa ukiwa na takwimu ili uzitoe lazima upate kibali cha NBS, jambo linalomaanisha kuwa zikiwa mbaya dhidi ya Serikali NBS watazuia.

Ni Mabadiliko ya sheria yaliyotulenga ACT Wazalendo, tuliyapinga lakini hatukusikilizwa. Sheria iliyolenga kutukomoa ACT Wazalendo athari zake zimekuwa kubwa mno kwa Taifa. Athari kubwa zaidi ni hatua ya Benki ya dunia (WB) kuzuia Fedha za mikopo na misaada zaidi ya shilingi trilioni 3 ilizopanga kutoa kwa Serikali kwenye miradi ya maji, elimu, na Takwimu, kwa sababu ya mabadiliko yale ya Sheria ya Takwimu ya mwaka 2018.

Jambo hilo la Benki ya Dunia kuzuia Fedha ndilo ambalo limeifanya Serikali ya Tanzania Mwezi Juni, 2019 ipeleke bungeni mabadiliko mengine ya Sheria ya Takwimu ili kuondoa vipengele ilivyoviweka mwaka 2018. Taifa limepotezewa muda na limepata hasara kwa sababu ya maamuzi ya kutukomoa ACT Wazalendo yaliyofanywa na Serikali.

Hali ya Ukuaji wa Pato la Taifa

Juni 16, 2019 tulifanya Uchambuzi wa Bajeti ya Nchi kwa mwaka 2019/20 ambapo tulionyesha mashaka yetu juu ya taarifa ya Serikali ya ukuaji wa uchumi wa 7% kwa mwaka 2018. Taarifa za Serikali yanyewe zilionyesha kuwa vichocheo vya ukuaji uchumi vimesinyaa, uwekezaji kutoka Nje (FDI) ukiwa umeshuka kutoka USD 5 Bilioni mwaka 2017 mpaka USD 2.8 Bilioni mwaka 2018, Misaada ikishuka kutoka Shilingi Trilioni 2.6 mwaka 2017 mpaka Shilingi trilioni 1.9 mwaka 2018, na urari hasi wa Kibiashara (Balanc of Payment Deficit) ukipanda kutoka USD 1.2 Bilioni mwaka 2017 mpaka USD 1.9 Bilioni mwaka 2018.

Lakini pia Uchambuzi wa takwimu za kasi ya ukuaji wa pato la mwananchi mmoja mmoja (Income per capital growth) na ukuaji wa pato la Taifa (GDP Growth) ulionyesha kuwa Serikali inapika taarifa, maana Muelekeo ulionyesha kuwa uchumi ulipaswa ukue kwa 5.6% tu kwa mwaka 2018 na sio hiyo 7% iliyosemwa na Serikali.

Benki ya Dunia imetoa ripoti mpya ya hali ya Uchumi wa Tanzania (Tanzania Economic Update) inayoonyesha kuwa kwa mwaka 2018 uchumi wetu ulisinyaa, na kuwa ukuaji wake ulikuwa ni 5.2% tu, na si 7% ya Serikali. Msingi wa ripoti hii ni taarifa za Serikali yenyewe. Ripoti hii ya Benki ya Dunia imetolewa ikiwa ni miezi kadhaa tangu Serikali izuie kutokewa kwa ripoti ya Shirika la Fedha Duniani (IMF) inayoonyesha kusinyaa kwa uchumi wetu na kuwa ukuaji wake kwa mwaka 2018 ulikuwa ni chini ya 5%.

Mapendekezo ya ACT Wazalendo

1. Ni dhahiri kuwa hali ya Uchumi wa nchi yetu si nzuri, malalamiko ya wananchi mtaani yanaonyesha hivyo, Mwaka 2018 hatukuuza korosho, hatukuuza tumbaku, na uzalishaji wa mazao hayo Makuu ya Biashara ulishuka, uzalishaji viwandani ulipungua kwa zaidi ya nusu, uwekezaji kutoka Nje ulishuka nk. Ni dhahiri kuwa kuna upikaji wa Takwimu kwa Lengo la kuonyesha kuwa mambo ni mazuri. ACT Wazalendo tunaona ni wakati sahihi wa kufanyika Uchambuzi wa wazi na wa Kina wa hali ya Uchumi wa Nchi yetu, Uchambuzi husika uhusishe Bunge, Serikali, Mashirika ya Kimataifa (IMF, AFDB pamoja na Benki ya Dunia) pamoja na Asasi za Kiraia, kwa Lengo la kupata uhalisi wa hali ya Uchumi wa Nchi yetu.

2. ACT Wazalendo tunalitaka Jeshi la Polisi lirudishe Simu, Komputa pamoja na vifaa vyote ilivyovichukua mwezi Novemba mwaka 2017 wakati wa mahojiano na Viongozi wetu pamoja na upekuzi kwenye Ofisi zetu. Ni miezi 18 sasa tangu wachukue vifaa hivyo, hawana haki kosheria kuendelea kukaa na vifaa hivyo.

3. Katibu Mkuu wa CCM awaombe radhi Watanzania kwa kutetea kwake takwimu za upotoshaji za Serikali, na kutunanga ACT Wazalendo tulipoonyesha kuwa Uchumi unasinyaa.

Dorothy Semu
Katibu Mkuu, ACT Wazalendo
Julai 21, 2019
Dar es Salaam
 
Noted!! Mapendekezo mazuri.......faragha ya mawasiliano ni muhimu kulindwa.
 
ACT wazalendo awali ya yote niwatakie kila lenye kheri mungu hamtupi MTU kwenye nia ya dhati. Ni wazi sasa yangu awamu ya tano kuingia madarakani licha ya kupata sifa kemkem toka kwa wananzengo na wachumia tumbo lakini hali ya mambo so shwari na matokeo take kila mwenyewe macho anaona raisi anapiga sarakasi kuwatisha watu huku uhalisia ukisalia pale pale mambo yamemshimda maana hata title project sake kama sgr na stieglers gorge there is deficit na juzi tu professor wa jalalani alikua China kula matapishi ya aliye mwita mpumbavu. Magufuli a wrong person in a right county
 
Back
Top Bottom