Katibu wa Idara ya Itikadi, Uenezi na Mafunzo wa CCM Zanzibar, Khamis Mbeto Khamis, amezindua rasmi Kituo cha Mafunzo ya Amali kilichopo Mbuzini, ndani ya Jimbo la Bububu. Kituo hiki kimejengwa kwa juhudi za Mwakilishi wa Jimbo hilo, Mudrik Ramadhan Soraga, kwa lengo la kuwawezesha vijana kupata mafunzo ya fani mbalimbali, ikiwemo ushonaji na ujasiriamali, ili kuwajengea ujuzi wa kujitegemea na kuinua maendeleo yao kiuchumi na nchi kwa ujumla.