Katibu Mkuu Ardhi aagiza vikao vya muda mfupi ofisi za ardhi kabla ya kuanza kazi

Joined
May 14, 2024
Posts
94
Reaction score
75
DODOMA

Katibu Mkuu Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhandisi Anthony Sanga ameziagiza ofisi zote za Ardhi nchini kuanzia mkoa hadi halmashauri kuhakikisha zinakaa vikao vya muda mfupi kila asubuhi kabla ya kuanza kazi ili kuwa na njia bora ya kutatua changamoto za sekta hiyo.

Amesema, utaratibu wa kuwa na vikao vya muda mfupi kila siku asubuhi kutawawezesha watendaji hao wa sekta ya ardhi kujua namna ya kushughulika na changamoto zinazojitokeza mara kwa mara katika maeneo yao ya kazi.

"Mnapokutana mnakaa kwanza vikao vifupi kila subuhi kabla ya kuanza kazi na kupanga mipango, hata kama kikao cha cha dakika tano ili kuona jana mlifanya kazi vipi na kuna changamoto gani ili mzishughulikie" amesema Mhandisi Sanga.

Soma Pia: Waziri Ndejembi aagiza Watumishi saba ardhi kuchukuliwa hatua za kinidhamu

Katibu Mkuu Mhandisi Sanga ametoa maagizo hayo tarehe 2 Desemba 2024 katika ukumbi wa Jakaya Kikwete jijini Dodoma wakati wa Maadhimisho ya Wiki ya Ardhi ambayo uzinduzi wake utafanyika rasmi
kesho jumanne tarehe 3 Desemba 2024.

Aidha, amewataka watendaji wa sekta ya Ardhi nchini kujitambua na kuelewa kuwa, watumishi wote wa sekta hiyo ni wamoja na wananchi wanajua kuwa wote ni watumishi wa Ardhi bila kuchanganua taaluma zao.

"Unapomuambia mwananchi ramani haijapanda yeye haelewi , usimtume mwananchi bali wewe msaidie, masuala ya ramani ni masuala yenu ya kitaaluma na tutoke katika tabia hiyo na kwenda kusaidia wananchi" amesema Mhandisi Sanga.

Kwa mujibu wa Katibu Mkuu Wizara hiyo
hatua kali zitachukuliwa kwa watumishi wa sekta ya ardhi watakaochelewesha huduma kwa makusudi.

"Hili ni jambo tunalolipiga vita sana, ni wasihi wakuu wa Idara kukagua kazi za wasaidizi wao kama ni kazi ikipokelewa itolewe".

Kwa upande wake Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Ardhi na Maendeleo ya Makaazi SMZ Bi Mhaza Gharib Juma amesema, Wiki ya Ardhi inayoadhimishwa itaimarisha mashirikiano baina ya Zanzibar na Tanzania Bara katika masuala ya sekta ya ardhi hasa ikizingaitiwa lengo kuu la serikali zote mbili ni kuisaidia jamiii.

Aidha, ametaka kuangalia namna sekta ya ardhi itakavyoweza kuimarisha masuala ya uwekezaji nchini kwa kuwa ardhi ni kila kitu na kusisitiza kuwekwa mikakati imara itakayoweza kutumia ardhi kwa uadilifu na haki ili kuimarisha uwekezaji na kupata fedha zitakazoongeza huduma mbalimbali kwa jamii.
 
Nani alizembea mpaka shirika la Nyumba likageuka kuwa mali ya wajanja na sio mali ya umma.
Wizara ya ardhi ina kazi gani wakati kila kitu kipo shaghala ba.ghala?

*Kwa nini serikali iwe nyuma ya wananchi badala ya kuwa mbele ?
Kwa Mujibu wa Comredi Bdugai Tanzania ni kati ya nchi zilizotolewa mfano na China kuwa ni sawa na farasi anayekokotwa na mkokoteni badala ya kinyume chake.

Unakuta mtu anajenga nyumba mpaka inaisha ndio anawekewa alama ya X.

Serikali ya hovyo inawatia umaskini wetu wake halafu insenda kuwapigia magoti wageni kuwaomba msaada wa kujenga vyoo vya mashimo.

Ni ilitegemea baada ya kuchagua wenyeviti wa serikali za mitaa wote wa CCM wangeweka utaratibu wa kuweka Ramani za kila mahali kwenye ofisi zote mpaka ngazi za chini .
Lakini pia Ramani za nyumba ziwe kila kwenye ofisi za serikali za mitaa . Watu wanapewa bure maana wanalipia kodi ya majengo waliyojenga bila msaada wa serikali .

Hii nchi haijapata kiongozi wa watu baada ya Nyerere na JPM zaidi ya watu waliobahatika kupata fursa ya utawala bila maono
 
Back
Top Bottom