PreGE2025 Katibu Mkuu BAKWATA: Serikali ifanyie kazi dosari za uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)

Waufukweni

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2024
Posts
5,383
Reaction score
18,776
Katibu Mkuu wa Baraza Kuu la Waislamu Tanzania (BAKWATA), Alhaj Nuhu Jabiri, amewahimiza wananchi kujitokeza kwa wingi kushiriki katika zoezi la uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura ili kutekeleza haki yao ya kikatiba.

Aidha, amezitaka mamlaka husika kuchukua hatua stahiki kufanyia kazi dosari zilizoripotiwa katika Uchaguzi wa Serikali za Mitaa uliopita na kuhakikisha haki inatendeka kwa wote.

"Kupitia jukwaa hili, tunaziomba mamlaka za Serikali kuzifanyia kazi dosari zilizoripotiwa katika uchaguzi wa Serikali za mitaa uliopita na kusisitiza suala la kutenda haki katika kila hatua ya mchakato wa uchaguzi, kwani haki ndiyo msingi mkuu wa amani. Tunatoa wito pia kwa vyama vya siasa pamoja na wagombea kuepuka vitendo vya rushwa, kwani rushwa ni adui wa haki"

Your browser is not able to display this video.
 
Chadema na kanisa la mwapinduzi watapinga
 
VIongozi wote wa dini wanapaswa kutokuwa wanafiki kama huyu Sheakh, watawala wanahubiri amani huku hawatendi haki...umeona wapi duniani ujinga kama huo!.
 
Kwa hili ameitendea haki dini ya mwenyezi mungu, haki kwa watu wote
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…