KATIBU MKUU CCM TAIFA NDG DANIEL CHONGOLO AFUNGA KAMBI LA UVCCM WILAYA MULEBA.
Kagoma, Muleba.
Katibu Mkuu wa CCM Taifa Ndugu Daniel Chongolo Katika ziara yake pamoja na Sekretrieti ya CCM Taifa Amefunga kambi la UVCCM lilioandaliwa na Uongozi wa UVCCM Wilaya Muleba Chini ya Mwenyekiti wake Mtwawafu Kantangayo. Kambi hili lilihusisha kujenga vyumba vitano vya madarasa ya Shule ya Sekondari Mpya ya BUKAMA - KAGOMA ambapo mpaka kufungwa kwake Vyumba vyote vilikuwa vimefikia usawa wa Rinta.
Katika Tukio hilo Mh. Katibu Mkuu aliambatana na viongozi wa Chama na serikali, wabunge na na madiwani.
Ndugu Katibu Mkuu wa CCM Taifa aliwakabidhi vyeti vya pongezi na kuwapongeza vijana kwa moyo wao wa uzalendo na kujitoa na hii imeonekana kama kuacha alama na mchango kwa Maendeleo Kwa taifa.
Aidha Alisisitiza kuwa kazi zote ambazo zitakuwa zikitokea ndani na nje ya Wilaya Muleba vijana waliojitolea wapewe kipaumbele na pia alitoa zawadi ya Shilingi Milioni moja kama motisha kwa kujitolea kwao. Na alihidi kwamba kundi hili la vijana atawapa kipaumbele na kuwasafirisha kwenda kufanya kazi katika mikoa mingine kwenye miradi ya Chama na Serikali ili kuwajengea uwezo wa kazi na kujituma.
Pia Katibu Mkuu Ndg DANIEL CHONGOLO Alisisitiza UVCCM kuendelea kuwa wamoja kwani kazi waliyoifanya ni kubwa na kuwaasa wanajumuiya ya UVCCM kuiga mfano Huo na kuacha mambo ambayo hayajengi Taasisi na Chama kwa Ujumla.
Habari hii imeambatana na baadhi ya picha za Matukio ya Ufungaji wa Kambi hilo.