Mkalukungone mwamba
JF-Expert Member
- Aug 29, 2022
- 862
- 1,755
Hamad ameeleza hayo wakati akichukua fomu ya Kugombea nafasi ya Uenyekiti Taifa wa chama hicho katika Ofisi za Wilaya ya Magharibi B Unguja
Amesema kila mwananachama atatumia haki yake ya kikatiba na Demokrasia katika kuchukua fomu ya kugombea nafasi hiyo ili kuendelea harakati za chama
Kuhusu Sababu za kuchukua fomu hiyo Hamad amesema ni pamoja na kutekeleza maombi ya Mwenyekiti wao wasasa Profesa Lipumba ya kuona kuna mabadiliko ya uongozi kwa ngazi zote ikiwemo Taifa
Wakati hayo yakiendelea hapo jana Tayari wapenzi na wafuasi wa Profesa Lipumba walifika katika Ofisi za CUF kumchukulia Fomu Profesa Lipumba kuendelea kulinda kiti hicho
Chama cha Wananchi CUF kipo katika mchakato wa kupanga safu ya Uongozi ambapo mwanzoni mwa mwezi wa Septemba wanatarajia kufanya uchaguzi kwa ngazi ya Taifa