TANZIA Katibu Mkuu Kiongozi, John W. Kijazi afariki dunia

Tatizo wabongo tu wabishi sana. Unakutana na mtu anakuambia Tanzania hamna Corona.

Unajiuliza kama mataifa mengine yote covid-19 ipo na inaua watu daily sisi Tanzania tuna ubia gani na Mungu mpaka covid isiwepo kwetu?

Ujinga huu huu ndio ulisababisha SA mpaka sasa AIDs ni janga kubwa. Kisa rais aliwaambia dawa ya ukimwi kuoga maji baridi.
 
Aisee nikiangalia idadi ya misiba nnayokutana nayo wiki mbili hizi
siyo hali ya kawaida

Something is not right somewhere
Toka mwaka jana mwezi wa 12 hali ni hiyohiyo mtaani kwetu watu wakasema oooh! Mungu anafunga hesabu yake ya mwaka, watu mnachanga nzengo mpaka mnachoka.
 
😆😆😆 Maji baridi !
 
Kuna huyo mtu anaitwa Mpango tumwombee.
Kuna huyo mtu anaitwa Gharibu Bilal tumwombee
Kuna huyo mkuu wa Magereza tumwombee
Kuna huyo mtu anaitwa Diwani Athuman sujui kama amepona.
 
Huna mchango wowote wa maana ni utopolo tu, mtu mwenye akili timamu hawezi kuwaza mambo ya kuvunja katiba ili fulani aongezewe muda kwa kipi hasa. Nenda kakojoe ukalale hujui chochote wewe
 
Mungu Wangu huyu baba kafariki. Hakika Corona itaondoka na mtu Ikulu.

This is more than breaking News.

Usiku wa leo Mh. Magufuli atalia kwa uchungu mno kwa kuondokewa na rafiki yake kipenzi.

Huwenda akabadili maamuzi yake dhidi ya CORONA.

Muhimu kubadili msimamo wako Mh Magufuli Inahusu maisha yako pia. Familia yako pia. Muhimu sana. Tunakuhitaji pia. Jilinde.

Wasaidizi wako wote (mawaziri) ndugu zako, RC, DC, everybody. Jirani zako,watu wako wa karibu, Tanzania nzima, ilinde.

Fanya uamuzi thabiti, waambie watu ukweli. Uamuzi thabiti. Ukweli.
 
Hilo CV reeefuuuu..... road engineering?

Tangible outputs hazionekani zaidi ya kujivika tu titles zenye masifa ya kisiasa!

Injinia Kijazi!
 
Hilo CV reeefuuuu..... road engineering?

Tangible outputs hazionekani zaidi ya kujivika tu titles zenye masifa ya kisiasa!

Injinia Kijazi!

Mkuu, heshimu waliokufa, wana familia. They mourn. Keep your stuffs for later time. Plenty of time to express yourself.
 
Tanzania tumepatikana aisee,Jamani turudie njia za kisayansi
Uswahilini bado watoto watu wazima wanajikusanya wanakaa vijiweni bila barakoa wala kunawa mikono huko ndipo kisimani maambukizi yote yamejaa
 
Sina cha kuandika zaidi ya kusema Tz hakuna Corona....but nadhan ngoma inakita mdundo ambao huwezi sikia sauti ya wimbo.
Ila hali ni tete kweli.

Wanaokufa viongozi wa huko juu ni dalili tosha kua huku chini hali ni mbaya sana
Wanaokufa pasipo kutangazwa ni wengi sana na hasa huko uswahilini kwenye mikusanyiko isiyo na umakini wala maonyo yeyote
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…