beth
JF-Expert Member
- Aug 19, 2012
- 3,880
- 6,368
Katibu mkuu wa Dayosisi ya Kaskazini ya Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) yenye makao yake makuu mjini Moshi, Arthur Shoo amefariki dunia katika Hospitali ya Rufaa ya KCMC alikokuwa akipatiwa matibabu.
Mkuu wa Dayosisi hiyo ambaye ndiye mkuu wa Kanisa hilo Tanzania, Askofu Fredrick Shoo amethibitishia Mwananchi Digital leo Februari 26, 2021 kuwa mtendaji wake huyo mkuu alifariki dunia jana usiku akiendelea na matibabu hospitali ya KCMC.
“Ni msiba mzito kwangu, familia na kwa wana Dayosisi wote,” amesema Askofu Shoo na kueleza kuwa alikuwa amelazwa katika hospitali hiyo inayomilikiwa na Shirika la Msamaria Mwema (GSF) tangu Jumatatu ya wiki hii.
Taarifa za kifo cha Katibu mkuu huyo zilianza kusambaa jana saa 3 usiku kupitia makundi ya whatsapp na Askofu Shoo alipoulizwa usiku huo alijibu tu kwa kifupi “Ni kweli usiku huu nimeondokewa na Katibu mkuu wa Dayosisi.”
Chanzo: Mwananchi