Katibu Mkuu Simba SC, afunguka kuhusu mipango ya Timu.

sembo

JF-Expert Member
Joined
May 25, 2011
Posts
4,350
Reaction score
3,451
Katibu Mkuu wa timu bora kwa sasa katika ukanda wa CECAFA, Simba SC, Ndg. Patrick Kahemele amefunguka mipango mbalimbali ya Mnyama katika msimu huu wa 2016/2017.

1. Ukusanyaji wa michango mbalimbali toka kwa wanachama
Patrick Kahemele ananena.. "Kuna kitu tumebuni kinaitwa, ‘crowd sourcing’, ambacho ni kuunganisha watu wenye nia moja kuchangia jambo fulani. Sasa hivi, teknolojia imekua hivyo tumeandaa mkakati wa kuwaunganisha wanasimba nchi nzima."
Patrick Kahemele anasema wao wameingia makubaliano na kampuni itakayotengeneza mfumo wa kiteknolojia utakaotumiwa kuwaunganisha mashabiki na wanachama wa klabu hiyo.
"Kampuni hiyo itatengeneza mfumo tunaita ‘USSD Code’, ambao utatumiwa na wanachama kuchangia michango na kuombea kadi za uanachama."

2. Kutafuta Mdhamini Mpya
Baada ya ule mkataba wa udhamini baina ya TBL na Simba S.C kuisha, timu ipo busy kusaka mdhamini mpya.
Patrick Kahemele anena..
"Kwanza udhamini wa TBL ulikuwa mdogo sana, nadhani sasa ni wakati muafaka kupata udhamini mkubwa zaidi, tayari tumepeleka proposal (dokezo) katika kampuni kadhaa na mazungumzo yanaendelea, pengine habari njema zitakuja hivi karibuni."
Ikumbukwe TBL walikua wanatoa milioni 500 tu kwa mwaka kama sehemu ya udhamini wao.

3. Posho kwa wachezaji msimu huu juu
Ili kuwapatia motisha wachezaji waweze kutimiza malengo ya kukomba Kila kombe lililo mbele yetu, posho imeongezwa maradufu tofauti na msimu uliopita.
Patrick Kahemele ananena..
"Msimu huu tuna malengo makubwa zadi hivyo tumekuja na mikakati mipya, hatutumii posho za mwaka jana maana hayo yalikuwa ni ya wakati mwingine na sasa ni nyakati nyingine."
Patrick Kahemele anaendelea.. ''..Wachezaji wanagawana posho kulingana na namna walivyocheza, waliovaa jezi wanapata posho kubwa zaidi ya wale ambao hawakuwa na nafasi, hii inaongeza ushindani ndani ya timu."

4. Ubunifu wa vyanzo vipya vya Mapato
Katika kuepukana na ile dhana ya kumtegemea mdhamini katika kila kitu, Simba S.C yaja na mradi wa kutengeneza pesa. Kwa kuanzia Mnyama kaanza na mradi wa kutengeneza maji yake.
Patrick Kahemele anena kuhusu hili.. "Tulichofanya ni kuipa tenda kampuni izalishe maji yenye nembo ya Simba tukiamini kuwa watu watashawishika kununua."..
Patrick Kahemele anaendelea kunena.. "Kampuni itakayotengeneza maji hayo itachukua pesa yake kama kawaida, ila wataongeza kiasi fulani kwenye bei ya hayo maji ambayo itaenda kwa Simba SC."

SIMBA SPORTS CLUB NGUVU MOJA
 
Mawazo murua tunahitaji usimamizi wa utekelezaji
 
Bora huyu awe hata Rais wa Simba kuliko kumpa timu MO

nimefurahi hajamtaja MO hapo

kama aliwapa Azam udhamini wa NMB huyu anaweza leta udhamini mkubwa zaidi na huyo MO aende zake
na utapeli wake
 
'timu bora
kwa sasa katika ukanda wa
CECAFA, Simba SC' ....sembo una maanisha nini hapo?
 
'timu bora
kwa sasa katika ukanda wa
CECAFA, Simba SC' ....sembo una maanisha nini hapo?
Hili swali haliko sawa, huwezi uliza unamaanisha nini, mtu anaposema kitu hiki ni bora, wewe kazi yako ni kiangalia vigezo vinavyo stahilli hicho kitu kuitwa bora je vipo, ulafu ukubariane nazo, ama ukatae. Sasa ukisema unamaanisha nini, inaonyeesha wewe hujui maana ya neno bora, labda ungeuliza kwa vigezo gani, maana unaweza usijue vigezo vya kitu fulani kuwa bora. Ama unataka kumpima huyo anasema hiki bora je anajua kweli vigezo kitu hicho kuwa bora.
 
Mara ya mwisho simba kuchukua kombe ilikuwa lini vile eti timu bora kwa sasa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…