Katibu Mkuu wa ACT Wazalendo, Ado Shaibu: Waziri Masauni ajiuzulu kwa kushindwa kudhibiti vitendo vya ukatili na uhalifu

Katibu Mkuu wa ACT Wazalendo, Ado Shaibu: Waziri Masauni ajiuzulu kwa kushindwa kudhibiti vitendo vya ukatili na uhalifu

The Sheriff

JF-Expert Member
Joined
Oct 10, 2019
Posts
747
Reaction score
2,112
Katibu Mkuu wa Chama cha ACT Wazalendo Ado Shaibu amemtaka Waziri wa Mambo ya Ndani Hamad Masauni kujiuzulu kutokana na kushindwa kudhibiti vitendo hivyo kutokana na kuongezeka kwa vitendo vya ukatili nchini.

Shaibu ametoa kauli hiyo wakati akizungumza na wananchi wa Kata ya Katoro, Wilayani Geita, katika mkutano wa hadhara akisema kwamba visa vya ukatili vinavyoendelea nchini vimekuwa vikilichafua taifa.

Miongoni mwa matukio hayo ni pamoja na watu kupotea kusikojulikana na wengine kufanyiwa vitendo vya kikatili kama ubakaji, hali ambayo inatoa taswira mbaya kwa taifa.

 
Back
Top Bottom