OKW BOBAN SUNZU
Platinum Member
- Aug 24, 2011
- 53,868
- 121,001
Katibu Mkuu wa Chadema John Mnyika yupo live akiongea na wanahabari kueleza mambo mbalimbali ya uchaguzi wa ndani wa Chadema na Uchaguzi Mkuu wa 2025.
Baada ya wagombea kuchukua fomu inafuata hatua ya usaili na uteuzi wa wagombea.
Anasisitiza wagombea kuzingatia maadili, miiko na muongozo wa chama dhidi ya rushwa. Kampeni zifanyike kwa uwazi haki na kuzingatia misingi ya demokrasia. Taratibu za kuendesha kampeni zinakataba kufanya kampeni kwa kuzingatia ukanda au ubaguzi wa aina yeyote ile.
Mgombea anakatazwa kutoa fedha au zawadi kwa wajumbe, kuwasafirisha wajumbe kuhudhuria kwenye mkutano, kushinikiza au kushawishi rushwa ya ngono, kutumia mamlaka ya uongozi.
Hata hivyo katika kipindi hiki cha uchukuaji na urudishaji fomu kumejitokeza vitendo ambavyo vinaashiria kuvunjwa kwa miongozo na baadhi ya wanachama mbalimbali kuna tuhuma za namna hiyo.”
“Iwapo kuna kiongozi au mwanachama au mgombea atakayeona yeyote anayekiuka miongozo hii aweze kuwasilisha malalamiko rasmi kwa Katibu Mkuu wa Chama au mamlaka za ngazi zinazohusika na anayetuhumiwa ili hatua ziweze kuchukuliwa kwa haraka ili kudhibiti hii hali ya kuwepo kwa ukiukwaji wa miongozo na taratibu za kampeni na uchaguzi.
Idadi ya Wagombea;
1. Mwenyekiti Taifa-3
2. Makamu Mwenyekiti Tanganyika-3
3. Makamu Mwenyekiti Zanzibar-4
4. Mwenyekiti BAVICHA-
5. Mwenyekiti BAWACHA-
6.Mwenyekiti BAZECHA-5
7. Katibu Mkuu-3