Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Katibu Mkuu wa chama cha Sauti ya Umma SAU, Majaliwa Kyara amesema ili kulinda maadili, kuimarisha malezi na kutunza nguvukazi ya Taifa, kuelekea mwaka 2050 ni muhimu wanawake waajiriwa wakawa na muda mfupi zaidi kazini.
Kyara amebainisha hayo Jumamosi Desemba 14, 2024 wakati akitoa maoni kwenye uhakiki wa Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050.
Katibu huyo amesisitiza kuwa watoto na vijana wanabaki wenyewe muda mrefu bila ya uangalizi wa wazazi, na hivyo kuwafanya kufuata tamaduni za kigeni wanazoziona kupitia mitandao ya kijamii.