Katibu Mkuu wa jukwaa la Mabunge ya nchi wanachama wa mkutano wa kimataifa wa kanda ya maziwa makuu (FP-ICGLR)

Katibu Mkuu wa jukwaa la Mabunge ya nchi wanachama wa mkutano wa kimataifa wa kanda ya maziwa makuu (FP-ICGLR)

Jamii Opportunities

JF-Expert Member
Joined
Feb 10, 2014
Posts
4,876
Reaction score
1,549
Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania linakaribisha maombi kutoka kwa Watanzania wenye sifa zinazohitajika kwa nafasi ya Katibu Mkuu wa Jukwaa la Mabunge ya Nchi Wanachama wa Mkutano wa Kimataifa wa Kanda ya Maziwa Makuu (FP-ICGLR). Nafasi hii itagombewa na wananchi kutoka nchi tatu wanachama ambazo ni Tanzania, Kenya, na Burundi, kwa mujibu wa maelekezo ya kikao cha TROIKA kilichofanyika tarehe 25 Oktoba, 2024.

MAJUKUMU YA KATIBU MKUU

Katibu Mkuu ataongoza Sekretarieti Kuu ya FP-ICGLR, na atakuwa na majukumu yafuatayo:

Kusimamia masuala ya utawala, fedha, na usimamizi wa kiufundi wa shughuli za Jukwaa;
Kuratibu shughuli zote za Jukwaa kwa mujibu wa makubaliano ya nchi wanachama;
Kutoa ushauri wa kitaalamu kwa taasisi mbalimbali ndani ya Jukwaa;
Kuhakikisha utekelezaji wa maamuzi ya Bunge la FP-ICGLR na mipango ya kimkakati ya Jukwaa.

SIFA ZA MWOMBAJI

Elimu:
Shahada ya kwanza (Bachelor's Degree) kutoka chuo kikuu kinachotambulika.

Uzoefu:
Uzoefu wa angalau miaka kumi (10) katika nafasi za uongozi wa juu katika taasisi za kitaifa, kikanda au kimataifa.

Uwezo wa Uongozi:
Sifa za uongozi, uadilifu, na weledi wa hali ya juu.

Jinsia:
Moja kati ya wagombea watatu wanaopendekezwa ni lazima awe mwanamke, kwa kuzingatia usawa wa kijinsia.

NAMNA YA KUTUMA MAOMBI

Waombaji wanapaswa kuwasilisha barua ya maombi, wasifu binafsi (CV), na nakala za vyeti vya elimu kwa njia ya barua pepe kupitia: cna@bunge.go.tz au

Ofisi ya Bunge,
10 Barabara ya Morogoro,
S.L.P. 941,
40490 Tambukareli,
DODOMA.


Tarehe ya mwisho ya kuwasilisha maombi ni Ijumaa, Machi 14, 2025.
 
Back
Top Bottom