Stephano Mgendanyi
JF-Expert Member
- May 16, 2020
- 2,833
- 1,301
ALIYOYAZUNGUMZA KATIBU MKUU WA UVCCM NDUGU KENANI KIHONGOSI AKIONGEA NA WANAHABARI AGOSTI 03, 2021.
Ndugu Kihongosi akampongeza Mhe Samia Suluhu Hassan kwa namna anavyoendelea kupambana vizuri na janga la Corona lililoikumba dunia nzima ikiwemo uamuzi wake wa kutoa chanjo za kujikinga na Corona na kuhamasisha wananchi kuendelea kuchukua tahadhari na kumhakikishia Mhe Rais Samia kwamba wao kama vijana wako pamoja nae katika harakati zake zote za kulinda afya za Watanzania.
Ndugu Kihongosi alitumia mkutano huo pia kumshukuru Rais Samia kwa namna anavyoendelea kuwaamini vijana na kuwateua kwenye nafasi mbalimbali za uongozi na kueleza kwamba wanaamini vijana watakwenda kufanya kazi iliyotukuka na kulinda imani ya Mhe Rais kwao.
Ndugu Kihongosi akaingia kwenye kiini cha Mkutano wake huo kwa kuanza kueleza kusikitishwa kwao kama Umoja wa Vijana wa CCM na kitendo cha vijana wa Baraza la Vijana la CHADEMA (BAVICHA) kuhamasishana kwenda mahakamani Tarehe 05/08/2021 wakaishinikize mahakama imfutie kesi Mwenyekiti wao Freeman Mbowe huku wakijua kitendo hicho ni kinyume na sheria.
Kihongosi aliwaeleza vijana wa CHADEMA kwamba nchi hii inaongozwa na Katiba na sheria za nchi na mambo yote yako kisheria hivyo wanapoingilia uhuru wa mahakama basi wajue wanavunja sheria za nchi huku akiwashangaa kwamba kama wao wanajipambanua wanataka demokrasia, wanataka mahakama iwe huru na ifanye kazi zake bila kuingiliwa, sasa inashangaza wao hao hao wanaita Waandishi na kuwahamasisha vijana wakaishinikize mahakama imfutie kesi Mbowe, wao hawana mamlaka hayo na kila muhimili unafanya kazi zake sasa wanapotaka kuingilia uhuru wa mahakama maana yake wanaingilia uhuru wa sheria zetu jambo ambalo halikubaliki.
Katibu Kihongosi akawaeleza vijana wa BAVICHA na Mwenyekiti wake (John Pambalu) kwamba wana wajibu wa kutii sheria na si kuwataka vijana kwenda mahakama kushinikiza mahakama.
Akawashangaa BAVICHA kutaka Mbowe afutiwe mashtaka wakati mahakama wala wao hawajajiridhisha kama Mbowe hana hatia? Kihongosi akawatolea mfano CHADEMA ambao juzi hapa baada ya Sabaya kupelekwa mahakamani walishangilia kwamba mahakama inatenda haki lakini leo wanageuka na kudai mahakama haiko huru. Kesi iko mahakamani halafu wewe unataka kushinikiza ifutwe, huo ni utovu wa nidhamu na Katibu Kihongosi akawataka kuheshimu sheria za nchi na kuacha mambo ya kitoto na siasa ambazo zimekosa hoja.
Kihongosi alisema inashangaza Ndugu Pambalu (Mwenyekiti wa BAVICHA) anasimama na kusema anamtaka Rais, hakuna mtu anayeweza kumtaka Rais, Rais yuko pale kisheria na anafanya kazi kwa miongozo iliyopo kisheria. Katibu Kenani aliwapa somo vijana wa BAVICHA. Rais ameshatoa msimamo kuhusu suala la Katiba, Rais kwasasa ana kazi kubwa ya kupeleka maendeleo kukuza uchumi kwa Watanzania nchi nzima, Rais ana wajibu wa kutimiza matakwa kwa Watanzania na sio hoja za mtu mmoja mmoja na wasaka vyeo.
Ndugu Kihongosi aliwashangaa vijana wa BAVICHA kudai Mbowe anaonewa bila ya kuwa na uthibitisho wowote. Akawataka kuviacha vyombo vya ulinzi na usalama kufanya kazi yake na kuacha kutweza jeshi la polisi, kudhalilisha mamlaka za vyombo vyetu vya ulinzi na usalama, jambo ambalo halikubaliki kwasababu hata hiyo amani ambayo wao wanaiona imesimamiwa na hilohilo Jeshi la polisi.
Ndugu Kenani alimtaka Pambalu kuomba radhi kwa kitendo chake cha kudhalilisha Jeshi la polisi na kumtaka kuliheshimu kwani ndilo ambalo limekuwa likimlinda yeye na familia yake akiwa amelala wakati Jeshi letu likiwa macho kulinda amani.
Aliwataka vijana wa CHADEMA kuacha kutumia ajenda ya Katiba kufanya uhalifu kwenye nchi yetu na kuwataka Watanzania kumpuuza Pambalu ambaye anataka kuharibu amani ya nchi yetu. Kihongosi aliwataka vijana kuendelea kutafuta kipato cha familia zao siku ya Tarehe 5 na kuacha kujiingiza kwenye migogoro ya kupambana na Serikali ambayo haiwezi kuongeza pato la nchi hii. Wanasiasa hawa wamesababisha matatizo kwa familia mbalimbali kama pale Arusha mtu alipata matatizo kwasababu ya hawa wanasiasa wa upinzani lakini wanasiasa hawa wanaendelea kudunda kila siku wakati wengine waliowahamisha vurugu wameumia na kuwataka vijana kukataa kutumika na wanasiasa walafi na waroho wa madaraka.
Ni lazima wananchi waendelee kutii mihimili ya nchi yetu na kuacha kutumika na wanasiasa ambao hawana cha kupoteza kwasababu wakiharibu hapa wanaweza kukimbilia nje ya nchi na wengine tunawaona wako huko Ulaya. Akili za kuambiwa changanya na zako na kutokubali kuingia kwenye mikumbo isiyo na tija kwa nchi.
Viongozi wa CHADEMA wana jukumu la kuwafunda vijana wao kuwa na adabu kwa mamlaka lakini wajue wanayoyafanya hakuna Mtanzania anawaunga mkono kwasababu kila wanapoitisha maandamano Watanzania wamekuwa wakiwapuuza.
Katibu alimaliza kwa kueleza vijana wa CCM wataendelea kuiunga mkono Serikali na kuwa mstari wa mbele kulinda amani ya nchi na kuwaeleza Watanzania kulinda umoja wetu. Wanasiasa wa upinzani wajifunze kwamba Watanzania hawashawishiki na siasa zao za chuki na uzandiki na ndio maana mara zote walipoanzisha kampeni za kuvunja amani na sheria hawajawahi kuungwa mkono na Watanzania. Wajishtukie. Mfano kwenye Ukuta, maandamano yao baada ya kushindwa uchaguzi mwaka jana hakuna aliyewaunga mkono.
Upinzani ujifunze kuridhika pale wanaposhindwa na sio kuilamu CCM ikishindwa kwasababu asiyekubali kushindwa si mshindani na wawe Mabalozi wa amani yetu. Toka Rais Samia aingie madarakani, ameendelea kuhamasisha siasa za upendo, umoja wa Kitaifa na zinazopeleka maendeleo kwa watu, cha ajabu wenzetu wa upinzani kutwa wamejizatiti kuhamasisha vurugu, uhasama na kuchonganisha wananchi na Serikali yao. Hili pekee linawafedhehesha na kuwaonyesha nia yao ovu kwa nchi hii.
Katibu Mkuu Kihongosi akamaliza kwa kuwataka wananchi kuendelea na shughuli zao za uzalishaji siku ya tarehe 05/08/2021 ambapo vijana wa CHADEMA wamepanga kwenda mahakamani kushinikiza mahakama imuachia Mwenyekiti wao basi watu wawapuuze na polisi wafanye kazi yao.
#MtumishiWaWote
#KaziIendelee
#TaifaKwanza