Katibu Mkuu Wizara ya Nishati, Felchesmi Mramba: Kupikia kwa umeme ni gharama nafuu kuliko vyanzo vingine vya nishati

The Sheriff

JF-Expert Member
Joined
Oct 10, 2019
Posts
747
Reaction score
2,112
Katibu Mkuu Wizara ya Nishati Mhandisi Felchesmi Mramba amesema hayo akizungumza leo Jumatano Agosti 7, 2024 alipotembelea banda la Wakala wa Nishati Vijijini (REA) lililopo katika maonesho ya Nanenane Nzuguni Jijini Dodoma.

“Wakati mwingine tunatumia umeme kuwasha taa, kuwasha TV, kuwasha radio, kuwasha AC na feni lakini hatutumii umeme kupikia kwa sababu tunaamini bei yake itakuwa juu sana lakini ujumbe ambao upo kwenye maonesho ya Wakala wa Nishati Vijijni (REA) ni kwamba sasa teknolojia imewezesha utumie umeme kupikia na gharama yake iwe ndogo kuliko kutumia vyanzo vyote vinavyofahamika”, amesema Mhandisi Mramba.

Soma Pia: Nishati Safi ya Kupikia, Mwarobaini tunao na ni Bora kuliko Gesi

Hayo yamesemwa na Katibu Mkuu Wizara ya Nishati Mhandisi Felchesmi Mramba akizungumza leo Jumatano Agosti 7, 2024 alipotembelea banda la Wakala wa Nishati Vijijini (REA) lililopo katika maonesho ya Nanenane Nzuguni Jijini Dodoma.

“Wakati mwingine tunatumia umeme kuwasha taa, kuwasha TV, kuwasha radio, kuwasha AC na feni lakini hatutumii umeme kupikia kwa sababu tunaamini bei yake itakuwa juu sana lakini ujumbe ambao upo kwenye maonesho ya Wakala wa Nishati Vijijni (REA) ni kwamba sasa teknolojia imewezesha utumie umeme kupikia na gharama yake iwe ndogo kuliko kutumia vyanzo vyote vinavyofahamika”, amesema Mhandisi Mramba.

Serikali ikipunguza bei za unit za umeme haitahitaji kutoa semina ya kuhamasisha wananchi juu ya kupika Kwa kutumia umeme. Watu watahamasika wenyewe BILA kuhitaji nguvu yoyote Toka nje
 
Anaongelea umeme huu!!?
Screenshot_2024-07-18-10-39-18-255_com.android.mms~3.jpg
 
Kwani unit 1 ya umeme shilingi ngapi?
Pia tozo za sirikali, pango la ardhi kupitia mita za umeme zinanyonya jumla shilingi ngapi kwa mwananchi wa kawaida?

Wacha tu tuendelee kutumia mavi ya ng'ombe yaliyokauka na hiyo hela ikanunue sukari kwa mangi japo nako zakayo wa tozo na maokoto kasimama kama mkuki kwa mganga wa kienyeji.
 
“Wakati mwingine tunatumia umeme kuwasha taa, kuwasha TV, kuwasha radio, kuwasha AC na feni lakini hatutumii umeme kupikia kwa sababu tunaamini bei yake itakuwa juu sana lakini ujumbe ambao upo kwenye maonesho ya Wakala wa Nishati Vijijni (REA) ni kwamba sasa teknolojia imewezesha utumie umeme kupikia na gharama yake iwe ndogo kuliko kutumia vyanzo vyote vinavyofahamika”, amesema Mhandisi Mramba.
Kwa kipato chake ni sawa siyo kwa watu wa kipato cha chini
 
Ni kweli kabisa ila kwa wanaotumia induction cooker. Haya majiko mengine yanalamba umeme haswa.
 
Serikali ikipunguza bei za unit za umeme haitahitaji kutoa semina ya kuhamasisha wananchi juu ya kupika Kwa kutumia umeme. Watu watahamasika wenyewe BILA kuhitaji nguvu yoyote Toka nje
Hakika!
 
I agree with ypu na kumbuka kwa umaskini wetu wakitz wanabid wajiandae kununua sufuria za umeme si chini ya 150k
 
Back
Top Bottom