Suley2019
JF-Expert Member
- Oct 7, 2019
- 2,203
- 5,610
Katibu Mwenezi wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA Jimbo la Njombe Mjini Emmanuel Kayombo na wenzake saba wamehama Chama hicho na kutimkia Chama Cha Mapinduzi CCM
Mwaka 2020 Kayombo aligombea udiwani Kata ya Njombe Mjini, Kupitia lakini hakufanikiwa kushinda. Na mwaka 2024 aligombea uenyekiti wa serikali ya Mtaa wa Kambarage ambako nako aliangukia pua dhidi ya Francis Msanga(FM) wa CCM aliyekuwa akitetea kiti hicho kwa awamu nyingine.
Zoezi la kuhamia CCM limefanyika leo January 4, 2025 Mjini Njombe na kupokelewa na Katibu wa Siasa Itikadi Uenezi na Mafunzo CCM Mkoa wa Njombe Ndugu Josaya Luoga ambaye amewataka kuanza kazi ya kukiimarisha chama hicho mara moja.
Akizungumza baada ya kukabidhiwa kadi ya CCM Kayombo na wenzake wamesema kilichowavutia kwenda CCM ni katiba imara na yenye misingi ya kuigwa pamoja na nidhamu kubwa iliyopo ndani ya CCM.
Aidha Kayombo amesema chama alichokuwepo kimekosa nidhamu na kuweka hadharani mambo ya kuyajadili ndani jambo lililomfanya atimkie CCM kwani hakuna yeyote anayeweza kufanikiwa bila kuwa na nidhamu.
"Taifa linashuhudia Chama kile cha (CHADEMA) kitu kinachoitwa utovu wa nidhamu, yani gari lile dereva na msaidizi wote wamelewa lakini vile vile hata baadhi ya abiria nao wamelewa kwa hiyo sisi wengine tukaona wanatuchanganya tumeamua kuondoka" amesema Kayombo