Pre GE2025 Katibu NEC, Mbeto: Pemba si mateka kwa Upinzani, Wanachama 2500 wa ACT wajiunga CCM

Pre GE2025 Katibu NEC, Mbeto: Pemba si mateka kwa Upinzani, Wanachama 2500 wa ACT wajiunga CCM

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)

upupu255

Senior Member
Joined
Sep 4, 2024
Posts
119
Reaction score
144
Chama Cha Mapinduzi (CCM) kimevunja mwiko wa kisiasa kudhani Pemba ni mateka wa upinzani na kwamba wanaweza kufanya watakavyo kwa kuendesha siasa za kufikirika.

Katibu wa Kamati Maalum ya NEC Idara ya Itikadi, Uenezi na Mafunzo, Khamis Mbeto Khamis, ameeleza hayo kufuatia wanachama zaidi ya 2500 kukihama ACT Wazalendo na kujiunga CCM.

1739857287299.jpeg
Mbeto alisema tokea mwaka 1995, upinzani umekuwa ukiifanya Pemba ni kichaka cha kufanya siasa za uongo , kupotosha dunia na kukigeuza kisiwa hicho, shamba la mapato binafsi ya wanasiasa wao wanaotajirisha.

Alisema kwa muda mrefu Pemba imetumika kubadili maisha binafsi ya wanasiasa wa upinzani wanaochaguliwa Udiwani , Ubunge na Uwakilishi huku wawakilishi hao wakishindwa kutatua changamoto za wananchi.

"CCM kimevunja mwiko wa kuifanya Pemba mateka wa upinzani . Kuna baadhi ya wanasiasa walidhani wangeifanya Pemba watakavyo. Wamewatumia sana wananchi ili kufikia matlaba yao .Zama hiyo sasa imepita" alisema Mbeto

Kupata taarifa na matukio yanayojiri kuelekea uchaguzi mkuu kwa kila mkoa ingia hapa: Special Thread: Mijadala na Matukio ya Uchaguzi Mikoa yote Tanzania Bara na Zanzibar kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025

Aidha aliongeza kusema kuwa utendaji wa Serikali ya awamu ya Nane Zanzibar chini ya Rais Dk Hussein Ali Mwinyi, imewafumbua macho wananchi wa Unguja na Pemba sasa wanafurahia mwamko wa maendeleo .

"Zama ya siasa za kuwagawa wananchi kwa Upemba na Uunguja imepitwa na wakati. Wazanzibari wanajitambua ni wamoja na hawatogawanyika au kudanganyika" Alisema Mbeto

Pia Katibu huyo Mwenezi , alisema mabadiliko ya miaka minne ya maendekeo toka Rais Dk Mwinyi awe madarakani ,uongozi wake umeleta mabadiliko makubwa ya maendeleo yanayoonekana unguja na pemba.

"Miaka mitano ijayo Rais Dk Mwinyi ataifanya za Zanzibar kuwa nchi inayotamaniwa na kila binadamu kuishi. Maendeleo yake yataishangaza dunia na kuwa kimbilio la kila mtu aidha kutamani kuishi , kuwekeza miradi au kutalii" Alisisitiza Mbeto
 
Back
Top Bottom