Roving Journalist
JF Roving Journalist
- Apr 18, 2017
- 3,984
- 13,760
Aidha amemuagiza Mkurugenzi Mtendaji wa Meatu kuhakikisha kuwa Mji wa Meatu unakua safi hatua itakayosaidia kupunguza kuenea kwa ugonjwa wa kipindupindu
Katibu Tawala Kayombo ametoa maagizo hayo katika Mkutano na Wananchi wa Kata ya Mbogayabanya wakati wa siku ya Usafishaji Duniani Kimkoa Wilayani humo.
Amewakumbusha Wananchi kujenga vyoo Bora na kuzingatia matumizi sahihi ili kuepuka kuenea ugonjwa wa kipindupindu.
Watu 47 wameripotiwa kupata ugonjwa wa kipindupindu katika Kata ya Mbogayabanya huku 3 wakipoteza maisha tangu kuingia kwa ugonjwa huo katika Kata hiyo.
Katibu Tawala Mkoa wa Simiyu, Prisca Kayombo alipokagua chanzo kimojawapo cha Maji Wilayani Meatu ,Moja kati ya shughuli aliyoifanya katika maadhimisho ya Siku ya Usafishaji Duniani Kimkoa Wilayani Meatu.
Pia soma:
~ Kihongosi: Baadhi ya Mila na Tamaduni zinachangia Kipindupindu Simiyu
~ Kipindupindu Simiyu kimeshamiri, kinaua ni hatari! Mbona Serikali haiweki wazi 'status' ipoje?
~ Wataalam wa Afya waingia mtaani kufanya jitihada za kudhibiti magonjwa ya kuhara Mkoani Simiyu