Katibu wa Itikadi na Uenezi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) mkoa wa Dodoma Jawadu Mohamed amesema baada ya vyama vya upinzani kushindwa kuteua wagombea wenye sifa katika baadhi ya maeneo, amedai zipo tetesi za vyama hivyo kujiandaa kususia na kulalamikia matokeo ya Uchaguzi wa Serikali za Mitaa.
Jawadu ametoa kauli hiyo Jumanne Novemba 26, 2024 katika kijiji cha Itololo, Wilaya ya Kondoa mkoani Dodoma wakati akifunga kampeni za Uchaguzi wa Serikali za Mitaa.