The Watchman
JF-Expert Member
- Nov 7, 2023
- 896
- 1,427
Katibu wa Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM) mkoa wa Pwani Comrade Iddi Ntonga amefanya ziara yake ya kazi wilayani bagamoyo ambapo ametembelea vikundi ambavyo vimenufaika na mkopo wa asilimia 10 ya vijana unaotolewa na halmashauri zote nchini.
Pia ametembelea vikundi vya waendesha Pikipiki maarufu BodaBoda na kuwatia moyo katika kazi zao.
"Umoja na ushirikiano na kufata sheria zote za usalama barabarani ndio nguzo ya usalama wetu, nasi kama viongozi tunaotokana na vijana tutajitoa kuwalinda na kuwatetea" Amesema Comrade Ntonga.
Aidha ametembelea Shule ya Sekondari Rupungwi iliyopo Kata ya Mandera Jimbo la Chalinze na kupata wasaa wa kuzungumza na wanafunzi kwa kuwasihi wasome kwa bidii na ili kutimiza ndoto zao na kuepuka wimbi la mmomonyoko wa maadili.