Mkalukungone mwamba
JF-Expert Member
- Aug 29, 2022
- 862
- 1,755
Mwili wa Mfanyabiashara aliyeripotiwa kupotea tangu December 11,2024 Jijini Dar es salaaam, Daisle Simon Ulomi, umekutwa katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Mwanyamala huku Uongozi wa Hospitali hiyo ukisema Ulomi afikishwa Hospitalini hapo December 11,2024 majira ya jioni akiwa ameshafariki na taarifa zinaonesha alifariki baada ya kupata ajali.
Kupata matukio ya nyuma kuhusu watu wasiyojulikana ingia hapa: Kiongozi wa Madaktari (Dr. Ulimboka) atekwa, aokotwa akiwa katika hali mbaya sana
Katibu wa Afya Mwandamizi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Mwananyamala, Lydia Nzema, ameiambia Ayo “December 11,2024 jioni tulipokea mwili kutoka Zahanati ya Makuburi, akiwa ameshafariki lakini Polisi kesi, ni kesi ya ajali mwili uliopatikana umepata ajali ameshafariki, ina maana alishapata kama ni matibabu au kama Kituo cha Afya alichopelekwa ilikuwa Zahanati ya Makuburi.
"Mwili ulikuwa Unknown hatukujua ni nani na tumehifadhi kwenye chumba cha maiti, leo December 16,2024 wamekuja Ndugu wameutambua mwili na wamesema ni Ndugu yao huyo Mfanyabiashara (Ulomi), kuhusu taarifa zaidi za alipata ajali gani taarifa zitakuwa mochwari zimeandikwa na taarifa zaidi Polisi wanazo.”
Soma Pia: