Binafsi sioni tatizo kwa sababu mawaziri ni wanasiasa na wanakagua utekelezwaji wa ilani yao. Kwahiyo kutembea na katibu wa ccm naona ni sahihi. Tunachokataa ni watendaji au watumishi wa umma kama TANROADS, TANESCO, etc kwenda kutoa ufafanuzi wa wanayoyafanya kwenye mikutano ya siasa ya ccm. Aidha kwa upande wa mawaziri ndo maana wadau wanapiga kelele kwamba mawaziri wasiwe wabunge. Kama mawaziri wasingekuwa wanasiasa, then waziri kutembea na katibu wa ccm hapo kidogo ingekuwa na walakini. Haya ndo maoni yangu wakuu.