Katibu wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Wilaya ya Mafia mkoani Pwani, Salehe Kikweo amefariki dunia wakati akiendelea kupatiwa matibabu Hospitali ya Mji Handeni, Mkoa wa Tanga.
Taarifa ya kifo hicho imetolewa na Katibu wa CCM, Wilaya ya Handeni, Mayassa Kimbau leo Jumanne Agosti 26, 2025 kupitia mitandao ya kijamii na kueleza Kikweo amefariki dunia asubuhi ya leo hospitalini hapo na mwili wake umehifadhia hapohapo.
Soma pia: Katibu wa CCM Wilaya ya Mbozi, Julius Mbwiga afariki Dunia
View attachment 3453764
Amesema taarifa zaidi kuhusu wapi yatafanyika mazishi yake itatolewa baadaye baada ya familia na viongozi wengine kukutana ili kupanga taratibu vizuri. Kikweo ni mwenyeji wa Handeni.
"Nimepokea kwa masikitiko makubwa sana taarifa ya msiba wa ndugu yetu, kaka yetu mpendwa Kikweo aliyefariki asubuhi hii ya leo na mwili umehifadhiwa Hospitali ya Bomani, mipango ya mazishi inaendelea kufanyika," imeeleza taarifa hiyo.
Akizungumzia msiba huo, Mwenyekiti wa CCM, wilayani Handeni, Amiri Changogo ambaye ni mmoja wa viongozi aliyefanya kazi na katibu huyo kwa muda, amesema kifo cha Kikweo kimetokea ghafla na wala hajaugua.
Novena imeanza kufanya kazi
Sisi tunataka nusu mlingotiNovena imeanza kufanya kazi
Alale pema tena mkuu...🤔Alale pema peponi kada
Na Allah akatende....😎Sisi tunataka nusu mlingoti
Ama kweli hiki chama kimechokwa aiseee...🤣Azikwe leo leo. Isifike kesho.
Heading wilaya ya MkurangaNi Mkuranga au Mafia?. Unatuchanganya wasomaji
Yaani wangelijua Kuna kifo wasingefanya haya wanayafanya kuligharimu Taifa. Hata huyu mama yao ipo siku ataondoka.Katibu wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Wilaya ya Mafia mkoani Pwani, Salehe Kikweo amefariki dunia wakati akiendelea kupatiwa matibabu Hospitali ya Mji Handeni, Mkoa wa Tanga.
Taarifa ya kifo hicho imetolewa na Katibu wa CCM, Wilaya ya Handeni, Mayassa Kimbau leo Jumanne Agosti 26, 2025 kupitia mitandao ya kijamii na kueleza Kikweo amefariki dunia asubuhi ya leo hospitalini hapo na mwili wake umehifadhia hapohapo.
Amesema taarifa zaidi kuhusu wapi yatafanyika mazishi yake itatolewa baadaye baada ya familia na viongozi wengine kukutana ili kupanga taratibu vizuri. Kikweo ni mwenyeji wa Handeni.
"Nimepokea kwa masikitiko makubwa sana taarifa ya msiba wa ndugu yetu, kaka yetu mpendwa Kikweo aliyefariki asubuhi hii ya leo na mwili umehifadhiwa Hospitali ya Bomani, mipango ya mazishi inaendelea kufanyika," imeeleza taarifa hiyo.
Akizungumzia msiba huo, Mwenyekiti wa CCM, wilayani Handeni, Amiri Changogo ambaye ni mmoja wa viongozi aliyefanya kazi na katibu huyo kwa muda, amesema kifo cha Kikweo kimetokea ghafla na wala hajaugua.
Usimpangie mungu. Siyo lazima amlaze pema peponi MEIZI WA KURA HUYU.Alale pema peponi kada