Mkalukungone mwamba
JF-Expert Member
- Aug 29, 2022
- 862
- 1,755
Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Kanda ya Nyasa kimewahimiza wananchi kujitokeza kujiandikisha kwenye daftari la mkazi ili waweze kushiriki katika uchaguzi wa Serikali za mitaa unaotarajiwa kufanyika baadaye mwaka huu.
Kauli hiyo imetolewa na Katibu wa CHADEMA Kanda ya Nyasa, Bi. Grace Richard Shio, alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari katika ofisi zake zilizopo Kadege, jijini Mbeya.
Bi. Shio alitoa wito kwa wananchi kutumia siku kumi, hadi Oktoba 20, kujiandikisha na kushiriki katika uchaguzi huo, akisisitiza kuwa kuchagua viongozi bora kwenye ngazi ya serikali za mitaa ni msingi wa maendeleo katika jamii.
Soma Pia: Ushauri toka kwa mpenda Demokrasia: Mmerejesha ngome yenu ya Nyasa. Pambaneni kanda ya ziwa 2025 mtafanya makubwa
“Ukiangalia, msingi wa maendeleo uko kwenye serikali za mitaa, vitongoji na vijiji. Viongozi tunaowachagua wanahusika na masuala mbalimbali ya jamii kuanzia usimamizi wa taka, masuala ya ndoa na hata tozo mbalimbali. Kwa hiyo ni muhimu kila mmoja wetu akajiandikishe kuanzia leo Oktoba 11 hadi tarehe 20, kuanzia saa mbili asubuhi hadi saa kumi jioni,” alisema Bi. Grace.
Alihimiza pia wale wenye uwezo wa kuongoza kujitokeza kugombea nafasi za uongozi katika vijiji, vitongoji, na mitaa kupitia CHADEMA, akibainisha kuwa chama hicho kimejipanga vyema na kina uhakika wa kushinda kwa zaidi ya asilimia 80 kwenye uchaguzi huo.
Hata hivyo, Bi. Shio alieleza kutoridhishwa na mwenendo wa zoezi la uandikishaji katika siku ya kwanza, akibainisha kuwa baadhi ya watendaji wa mitaa, vijiji, na kata wamekuwa wakisimamia uandikishaji kinyume na kanuni za uchaguzi, hasa katika maeneo ya Mbarali, Kalambo, na Kilolo, mkoani Iringa.
"Zoezi limeanza, lakini kuna changamoto kadhaa. Kanuni ya 10:3 ya uchaguzi inasema watendaji wa mitaa na kata hawaruhusiwi kuandikisha wapiga kura, lakini bado wamekuwa wakihusishwa katika vituo vya uandikishaji, jambo ambalo ni kinyume cha sheria," alisema Bi. Shio.
Aidha, aliwasihi wanachama wa CHADEMA kuendelea kushikamana na kuishi falsafa ya "CHADEMA ni nguvu ya umma" kwa kuhakikisha wanashiriki kikamilifu kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa na kujiandaa kwa uchaguzi mkuu wa mwaka 2025.